Tuesday, February 9, 2010

Maisha haya na mwanamke!

Japo mwanamke anaonekana au anaoneshwa kuwa chini, lakini kiuhalisia bila mwanamke maisha yanatisha zaidi. Mwanaume kama mpanda mbegu, kazi yake huishia kwenye milia ya misuguano na kifuatacho huwa ni kazi ya mwanamke. Mwanamke anabeba mimba kwa miezi tisa, hata baada ya mtoto kuzaliwa, mtoto huyo haunza kwa kuula mwili wa mwanamke kwani ni kwa kifua cha mwanamke, mtoto hujipatia chakula cha kutosha kwa siku nyingi bila wasi wasi. Mtoto hufurahia chakula hicho. Hata akikua uendelea kupikiwa chakula bora na mama yake. Tunaweza kuona tofauti dhahiri juu ya chakula kilichopikwa na mama /mwanamke au kilichopikwa na mtu mwingine. Hata wale wanaume wasiooa, maisha yao ni magumu kulinganisha na waliooa hata sayansi imelidhitisha hili. Lakini pia ukitembelea nyumba isiyo na mwanamke hata iwe safi lazima utahisi mapungufu uwapo pale, linganisha maisha ya kijana mwenye rafiki wa kike na aliyesingo! Utaona tu Sasa ndugu zangu, linganisha wale watoto waliolelewa na mama na wasiolelewa na mama. Inasemekana kuwa watoto ambao hawakulelewa na mama wana matatizo kadha wa kadha likiwemo la kutotii sheria na kutokuwathamini sana wakubwa, nikiwa mmoja wao nimeliona hilo na mengine na shukrani ni kwa mwalimu wangu wa utambuzi! Mwanamke ni kiumbe muhimu sana na adimu pia. I LOVE THEM

11 comments:

chib said...

Hii post.... mengine tutajaribu kuyafanyia uchunguzi!
Big up Kamala, siku hizi umeamia mwanza kabisa au...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kote kote, Bukoba, Mwanza, Musoma nk

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

kweli eh!

Umesema kuwa wanawake ni muhimu sana na YOU LOVE THEM!

hivi na wale wanaozaa na kutupa watoto nao unawamaindi?

Mija Shija Sayi said...

Kazi nzuri Kamala, Yaani tangu uoe naona unaanza kuyaelewa maisha ya mwanamke vilivyo hongera kwa hilo. Na bado ukipata mtoto ndo utakuwa unamwamkia kabisa mkeo na stori za mama zitapungua na kuhamia kwa mtoto na ni hapo ndipo utakapogundua kwamba mtoto si wa wote bali ni wako na mkeo.

@Chacha, wale wanaotupa watoto wanapojifungua huwa wamepatwa na Postnatal Depression. Unapokuwa na mimba homoni hubadilika (laiti kama ungependelewa na Mnyazi kupata mimba siku moja ili tu, ujue mvurugano wa homoni mwilini maana yake nini..)

Ndiyo maana Mrs Ngw'anambiti akiwa mjamzito ni tofauti kabisa asipokuwa mjamzito. Sasa ukijifungua hasa hasa miezi ya mwanzoni mvurugano wa homoni ndo huzidi kabisa na kumfanya mama kuwa kama amechanganyikiwa, hapa ndio utakuta wazazi wengi kama hawana usimamizi mzuri hutupa watoto wao au kwa Ulaya huwatoa kwa watu wengine walelewe ndiyo maana baada ya muda homoni zinapotulia huanza kujuta kwa nini walitupa watoto au kutoa kwa watu wengine.

Inabidi tuwapende tu hata hao watupao watoto.

Yasinta nesi wetu naomba utusaidie katika hili.

nyahbingi worrior. said...

kamala sikubali hata kidogo.

Nukuu

Hata wale wanaume wasiooa, maisha yao ni magumu kulinganisha na waliooa hata sayansi imelidhitisha hili.

Kwanza ni sayansi ipi ambayo imetumika ili tuafikiane na hili?

pili..Maisha yanakuwa magumu kivipi?

Tatu,mimi sijao na nia ya kuoa ninayo ingawa umri umenitupa mkono kidogo lakini.........

ndugu Kamala ni mwanamke yupi ambaye atakubali kuzaa nami taifa la wana wa Israeli?

Mija Shija Sayi said...

Nyahbingi, Kuhusu mwanamke atakaye kubali kuzaa na wewe.

Nadhani unakosea mawindo yako kakangu, wanawake unaowataka wapo ila hawaishi mazingira unayoishi. Unataka mwanamke atakayelikubali jembe, basi mfuate kwenye majembe vinginevyo hapo Kinondoni hutampata mtu.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Da Mija: inategemea ni majembe ya namna gani anayotaka. Ninaamini hata hapo kinondoni walimaji wapo...lol


inategemea ni kinondoni gani unaisema kwani ziko nyingi...lol

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@damija, asante kwa kumjibu Chacha na Nyabingi

ila kwa Nyongeza ndugu nyabingi kuna mtu kwa ajili yako, ila ukijiaminisha kuwa hayupo basi hatakuwepo kweli.
mimi ni vegeterian na ni meditator, nilikuwa najiuliza itakuwaje kumpata mwanamke kama huyo au wa kwenda na mimi? nikakutana na binti mlokole, tukakubaliana kuwa kila mtu ataishi bila kulazimishwa na mwingine kufuta imani au chakula, Ajabu, baada ya miezi michache yule mama akakop na kuanza kufuata imani yangu nk,\
usiseme hawapo

kuhusu sayansi, naomba nisiingie kupekua, ila wewe endelea kuwa singo tu, ukianza kujuta, rejea hii post na uitumie kuwaonya wengine!

@damija, umenijuza mengi maana napitia kipindi cha kuona mabadiliko kwa wife

mumyhery said...

Kamala Shukran kwa kuyajua hayo!!!

Anonymous said...

Hey
Companies House Webcheck
Webcheck Companies House
Company House Webcheck
Companies House Webcheck Service

[url=http://perosnalbinking.v3host.be/companies-house-webcheck.html]webcheck companies house[/url]

chib said...

@ Da Mija, umenichekesha na mtazamo wako wa Kamala kuoa. Nakubali Kamala anamwaga sera hasa kwa sasa!
Ila, sidhani naye atakubali ati wakipata mtoto basi shikamoo zitakuwa nje nje kuoka kwa Kamala kwenda kwa mamsap :-)