Tuesday, February 23, 2010

mwanamke na chakula--hitimisho

naomba kuhitimisha yale niliyokuwa nayo juu ya mwanamke, nahitimisha kwa kuangalia mwanamke na chakula alacho.

mwanamke anajiona wa kisasa leo na hivyo kulazimishwa na mazingira au kalazimisha kula chakula cha kisasa, kitamu, cha viwandani nk. mwanamke huyo basi anajikuta akiwa namatatizo lukuki ya kiafya yatokanayo na kula vyakula visivyostahili.

kijwe hiki hakitatoa ushauri juu ya ni chakula gani ale mwanamama kwani kilishafanya hivyo mwaka jana, ila kinamshauri mwanamama kuwa mbaguzi wa chakula ili kuilinda jamii nzima.

ila mwanamke naanywe maji mengi zaidi la lita tano kwa siku ili kuwalinda watoto wake na kujiletea furaha kati yake na Mume wake zaidi na zaidi.

huu ndio mwisho wa mada juu ya mwanamke, mada mchanganyiko zitafuata

7 comments:

chib said...

Ni hitimisho tu kwa sasa, najua sio mwisho wa mada hii.
Tunashukuru mkuu

SIMON KITURURU said...

Na MWANAMKE ajihadhari na hayo maji lita tano kwa siku kama ni mwoga kuchimba dawa maporini mchana au KUCHIMBA sumu usiku kama ataongozana na Komandoo Kamala katika misafara yake!
:-(

Chakujiuliza tu ni , ni jinsi gani chakula cha MDADA kinaulazima wakutofautiana na cha MKAKA wakati bajeti yenyewe kwa kawaida ndiyo hiyo tena IMEKONDA nyumbani kwakina Mwaniwane walio wengi?

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

duh! lita 5?

kwa dunia ya sasa ambapo maji ni anasa ni wachahe wawezao kuyapata kama ilivo kwa chakula cha kutafuta kwa manati :-(

Mija Shija Sayi said...

Kamala unataka kutuua, lita tano?? au umesahau kwamba kunywa maji mengi sana pia ni hatari kuliko hata kutokunywa kabisa? Maji mengi hupunguza kiwango cha chumvi katika damu na hivyo unakuwa hatarini kuzua matatizo mengine makubwa.

Lakini hata hivyo naungana na Mzee wa Ukala a.k.a Chib, hii makala umeikatisha wajameni.

Stay blessed.

Anonymous said...

Kweli hii blog yako imetulia kaza uzi ndugu yangu. Big up san.

www.ajirazetu.blogspot.com/ wwww.harusiyetu.blogspot.com.

mumyhery said...

acha tupumzike kidogo!!!

Yasinta Ngonyani said...

Kweli kabisa asemavyo D mija lita tano za maji Kamala unataka kutuua kabisa. Na hivyo vyakula kwa nini vitofautishwa?