Monday, February 1, 2010

Mwanamke na uana-uke wake,

Viumbe vya kike vinaitwa hivyo kwa sababu ya kuwa na umbo maalumu laiitwalo uke, hili ni tofauti na mwili mzima na hivyo ni kijisehemu kidogo tu ambacho mara nyingi hukaa nyuma (kwa wanyama watembeleao miguu na mikono) lakini hukaa katikati ya mapaja kwa viumbe watembeleao miguu miwili yaani wanadamu.--- definition hiii ni yangu binafsi!
Kwa hiyo mwanadamu aitwaye mwanamke ni yule mwenye uke, na mwanamume ni yyule mwenye uume. Uke unaonekana kwa macho ya haraka kuwa na kazi muhimu tatu; kukojolea, kuingiziwa uume, na hata kuzalia. (wote /wengi tulipitia ukeni!). Hata hivyo kuna kazi nyinginezo kama kutolea uchaufu wa hedhi, kuburudisha! Nk
Katika jamii zinazofuata imani za dini za mapokeo hasa kutoka Uarabuni na Roma via Ulaya, mwanamke anaonekana kuwa kiumbe asiyefaa. Ukiangalia wakuu wa dini huwa ni wanaume na hata waanzilishi wake. Hili tutaliona baadaye. Biblia (labda na korani?) zinatuaminisha kuwa mtu wa Kwanza yaani Adamu ndiye aliyetoa Eva (mwanaume)
Tunaambiwa kuwa Adamu alisinzia na kumtoa Eva. Lakini Ushahid tulionao leo ni kwamba wewe, mimi na yule, sote tumetokea tumboni mwa mwanamke, tena kwa kupitia Ukeni!
Hivyo basi, hata mbele ya maumbile, mwanamke ni mtu muhimu saana kuliko maelezo. Hata uwezo wa yule aitwaye Mungu, kuweza kuumba, unategemea uwepo wa mwanamke. Bila mwanamke ni vigumu kwa watu kuongezeka duniani. Mwanaume mmoja anaweza kuzalisha wanawake wengi kuliko kinyume chake. Hivyo mwanamke ni muhimu kuliko tunavyoweza kuongea na ushaidi wangu na wewe wa kuona na macho yetu kuliko ule wa kiimani ni kwamba, malamute ( na uume wake) na mwanamke wanatokeea kwenye tumbo la mwanamke
Chacha anadai kuwa labda mwanamke aliitwa hiyo kutokana na kuwa na tumbo yaani WOMB-MAN, labda! Ila ikumbukwe kuwa sio tumbo tu, bali tumbo muhimu ambalo mimi na wewe tuliwahi kuishi, kukaa na kuijia duniani.
Ni hayo kwa leo

10 comments:

Mija Shija Sayi said...

Umeongea kweli Kamala, Sasa huyu mwenzetu Caster Semenya unamuweka katika kundi gani? Mwanamke au Mwanaume?

Yasinta Ngonyani said...

Ni swali nzuri da Mija naungana nawe, Kamala twaomba jibu:-)

Munale said...

Hata katika maendeleo,ukita
ka kujua jinsi jamii fulani ilivyoendelea angalia jinsi
wanawake wa jamii hiyo
walivyoelimika.

Candy1 said...

Quoting "Hivyo basi, hata mbele ya maumbile, mwanamke ni mtu muhimu saana kuliko maelezo."

AMEEEEEEN!!! Yaani a MAN who talks sense about women, nimependa kweli!

Hehehehe dada Mija...doh...hata mie nasubiri jibu

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Duh

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

swali ni zuri sana, ila namimi nina swali, who is Caster Semenmya???

anaweza kuingizwa uume au kuingiza kwa wengine? ana uke au uume?

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Kamala & Da Mija: Inategemeaa kipi kati ya hizo alizo nazo kinafanya kazi zaidi ya kingine.

Nakumbuka katika mji mmoja hapa mkoa wa Mara kulikuwa na ntu mmoja ambaye walikuwa wanamuita SOFIA (sio jina lake halisi). huyu bwana (zamani ningesema DEMU) akiwa shule ya msingi alileta kizaizai mtaani.

Wazazi na majirani walijua ni binti japo alikuwa nazo mbili-ya kiume na ya kike :-( (sina hakika zilikuwa zimejipangaje hapo kwa kuwa sijawahi kuona....lol!!!) Kwa kuwa alikuwa na matiti(na bado anayo) na kasauti mwororo.

Basi nyumba ya jirani kukawa na wageni na kwa kuwa kwao huyo njemba kulikuwa na nafasi wageni wakapewa chumba cha binti na wazazi wa binti wakaja kwa jirani ambako kuna JIKE-DUME (JD) kuomba hifadhi ya binti yao mpaka wageni watakapoondoka! Wazee wa JD wakakubali na binti akaja kupiga mausingizi kwa sana hapo homu kwa JD kila jioni.

Duh! Ni wakati huo ambapo ilipogundulika kuwa si JD bali DUME-JIKE (DJ) kwani siku ya kwanza tu alipokuja huyo kigoli ambaye alikuwa hajamjua mwanaume DJ likaomba KUMUONJA. binti akasema UTANIONJAJE nawe ni kama mimi? :-(

Njemba ikasema...ni kweli ninazo mbili lakini gear leaver inasimama kuliko kile kibakuli kudai kuonjwa :-( Binti akasema no sweti ngoja nione....AKABIKIRIWA na wakati akiendelea kuonjwa siku za kijani zikafika AKAPATA MIMBA!

Ninavoongea jamaa alioa baada ya testimoni ya binti na madaktari :-(

Hivo huyo Semenya naye atwambie kipi kinafanya kazi-kama ni JD niende nimtokee :-( Kama ni DJ nimpelekee mwanangu wa kike ili nipate mang'ombe :-)

Yasinta Ngonyani said...

NIMENUKUU "Hivo huyo Semenya naye atwambie kipi kinafanya kazi-kama ni JD niende nimtokee :-( Kama ni DJ nimpelekee mwanangu wa kike ili nipate mang'ombe :-)" haswaaaa????

Mija Shija Sayi said...

Sasa kwa semenya inakuwa tofauti kidogo yeye ni mwanaume ndani ya mwili na mwanamke nje.. unaona utata huo?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

basi ni mwanamke mwenye mimba ya mwanamume.

lakini yawezekana anapakaziwa kwasababu aliwashinda wanawake wa kidhungu!