Saturday, February 13, 2010

ni mwanamke na uongo, udanganyaji, maisha feki.


katika mada juu yamwanamke, sasa tunaangalia jinsi mwanamke alivyokuwa mwongo na sio halisia kama atakavyoieleweke.


kuna ubishi kuwa wanaume udanganya sana kuliko wanawake, ishu ni kwamba wanaume huuishi uongo wa hapa na pale, kwa mfano mwanaume atakwambia niko saloni kumbe yuko bar, au niko kwa jamaa kumbe yuko nyumba ndogo nk


sasa mwanamke, utamwangalia, na kuzipenda nywele zake na unadanganyika na kumsogelea, kumbe sio nywele zake, ni kiwigi kavaa kichwani au kashonea nywele za bandia, duh!


utamwangalia na kuipenda ngozi yake, kumbe sio yake, kapakaa wanja, au kajichubua. unamwangalia midomo, myekuuuuduuu, kumbe yakwake inatia aibu, kapakaa tu kijiti cha cha lip (lipstick)


unamwona mdada na kuupenda urefu wake, kumbe sio mrefu wala nini, kavaa kiatu kimemtangulia na ukimwangalia miguuni utadhani anashuka ngazi mbili kwa wakati mmoja.


wakati mwingine unaaangalia matako, unavutuia, kumbe uswahili mmtupu.


maziwa ya mama mtu mzima yamesimama, unavutiwa, kumbe sio yake wala nini ila kavaa miplastiki ndo iliyosimama hata yeye hana amani, inamuumiza mradi umuone mrembo (onyo! usiniulize nimejuaje)


sauti nyororo, akiongea utadhani maneno yanatoka kwa malaika, kumbe anaigiza, sauti yake ni kibesi, mikwaruzo utadhani unaongea na mwanaume mwenzio nk nk


uongo gani unaujua audanganyao mwanamke?


mada inaendelea, tutaona juu ya chakula kwa mwanamke, then urais wako kutoka kwa damija

7 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Ama kweli ukistaajabu ya Kamala utaona ya ....!

mbona hujasema juu ya wanawake wanaochezea hisia za wanaume? Kwa kuwa nakasikiaga kuwa wanawake wengine wakishajua waume wanawapenda basi hucheza na hisia zao kama wanavopepeta nchele kwenye ungo...lol

Yasinta Ngonyani said...

nanukuu "sauti nyororo, akiongea utadhani maneno yanatoka kwa malaika, kumbe anaigiza, sauti yake ni kibesi, mikwaruzo utadhani unaongea na mwanaume mwenzio nk nk" mwisho wa kunukuu

kweli ukistaajabu ya kamala utaona ya.....

mumyhery said...

Naona leo umeamua kuwachambua kama karanga!!!

chib said...

DUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUH!!!!

Nuru Shabani said...

Haya Kaka, Ni kaazi kwelikweli.

PASSION4FASHION.TZ said...

Haya we tuchambue tu kama karanga,sisemi kitu sababu umetoa onyo kabla ili usiulizwe umejuaje?

Mgole hajambo lakini?
mpao!

EDNA said...

Hahahaa hujatulia kabisaa,Yaani ndio unatuchambua namna hii jamani,Lakini jamani vipodozi na vikorombwezo vingine si vimewekwa ili mwanamke avitumie? wacha tujikwatue bwana!! maamna tusipojiremba mtasema pia.