Thursday, February 18, 2010

salaamu kutoka geita!

nawaletea salamu lukuki kutoka geita, jiji la dhahabu, kuna dhahabu lukuki japo umasikini kama kawa, mji huu umekalia dhahabu ya kufa mtu.

maisha hapa ni mazuri na hali ya hewa ni kama Bukoba japo hapa udongo ni tope na mbu sio wengi kama kule kwetu bukoba.

migodi inatuharibia mazingira lakini ndo iyo mawe tulakolaki?

mada juu ya mwanamke itakuijia baada ya safari hizi ndefu.

Omulangila, kamala Lutatiinabigambobyabyantu

6 comments:

Candy1 said...

Hiyo ndio home sweet home lakini sehemu ambazo zimejaaliwa madini (particularly Africa), zote si zipo hivi jamani au?

Stay safe kaka.

Anya said...

I wish I was there ....
It looks BEAUTIFUL so peaceful :-)

(@^.^@)

Yasinta Ngonyani said...

Kamala naona tubadili ratiba mimi nije huko badala ya wewe kuja huku au unasemaje?

Mija Shija Sayi said...

Yasinta na hii winta ya safari hii mbona humtakii mema Kamala? labda kama ana mpango wa kuja huko summer.

SIMON KITURURU said...

Niliipenda sana Geita nilipoitembelea mwaka juzi!

Ila mwenyeji wangu alinitisha sana kwa statistics alizonielezea za jinsi UKIMWi unavyokua tokea WACHIMBA DHAHABu waongezeke hapo na HALI hiyo hasa inaunganishwa na miserebuko ya wachimba MADINI baada ya kazi.

Kwa kifupi tisha toto yake ilikuwa inaenda mkao wa :

JIADHARI na YEYOTE anayevutia HAPO kwa kuwa burudani kubwa hapo ni POMBE na NGONO na WAZURI katika mzunguko mdogo wa watu HAPO ndio walengwao kwa juhudu katika tumbuizo kwanza.


Na cha ajabu mji tajiri kama huo nilikuta shida ya maji na pia mpaka watu washindwao kupeleka watoto wao SHULE.

Maji yakutoka ZIWANI yanaenda mgodini lakini kwa wananchi hayapitii.

Hivi barabara imeshamalizika kutengenezwa?

Najua lakini wenye mgodi hawaji kwa gari labda barabara wala haiwahusu.:-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@Candy, Asante @anya, welcum
@yasinta, wewe unatakaje, amua tu lakini kumbuka mwenda kwao si mtoro, njoo tu

@Mijashija, You neva know, sometimes baridi yaweza kuwa njema, si unajua nimelazimika kukimbia joto la da na kwenda kwenye baridi mikoani??

@kitururu, ni kweli, si unajua maisha ya wachimba madini yalivyo? shida ya maji iko pale pale na omba omba wa kutosha ila wajenzi wa baa na guest hse ni wataalamu haswaaa

kwa bahati nzuri barabara ya Bukoba ni lami kutokea geita, na ile nyingine ni lami mpaka Senge-rema, nimeshangaa ilivyokamilika kwa haraka hivi