Friday, March 26, 2010

akili akili ni nini??

eti akili ni nini?? damija kasema waHaya tuna akili, sijui akili ni nini jamani, au inamaanisha nini??

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Akili ni nywele na kila mtu ana zake. wahenga walisema hili:-)

chib said...

Waweza kuwa na akili nzuri au mbaya. Hii ni tafsiri yetu waswahili.
Ukitazama upande fulani wa akili ya mtu, basi ndio utamuona na akili hiyo unayoitazama

Mija Shija Sayi said...

Kwa mtizamo wangu akili ni uwepesi wa kuelewa mambo na mgumu wa kusahau, yaani kuwa na ubongo wenye nguvu zaidi ya sumaku.

Kamala swali hili ulilotupa ukianza kulitafakali sana unasikia kuchanganyikiwa. Hebu angalia Braza Chib alivyofafanua.

Anonymous said...

Kwa matumizi ya Watanzania tuliowengi, ni uwezo wa darasani. Lakini katika hali ya kawaida mie nadhani akili uwezo wa mtu kujitambua yeye ni nani na kuwa na msimamo pasipo kuyumbishwa na mtu. Pia kutumia rasilimasi chache zilizopo kuweza kubadilisha maisha yake badala ya kubaki anajilaumu(maana nyingine ni mtu anaekubali matokeo kutokana na hali aliyonayo na kuchukua hatua kutoka katika hali aliyonayo

Kapongo said...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@Yasinta, unamaanisha ndo sababu wanawake hutafuta mpaka nywere za bandia??

@Chib, waweza kuwa sahihi katika mtizamo wako

@damija sijui!

@kapongo, kuna asiyeyumbiswa ulimwengu huu kweli? rasilimali kweli ubadili maisha na kuondoa lawama? ni akili kweli?

John Mwaipopo said...

siko mbali saana na kapogo (anonimasi). uwezo wa kugeuza magumu yalainike na yamfae mhusika binafsi na jamii inayomzunguka.

@kamala nasubiri comment!

Tandasi said...

akili ni uwezo wa ubongo kupambanua, kukariri,ili kuleta suluhisho