Monday, March 15, 2010

kipa na mpira --- kichekesho


moto uliwaka ghorofa ya saba katika jengo moja lenye ghorofa tisa nchini uingereza, watu wote waliruka chini, na katika ghorofa yanane alikuwamo mama mmoja mwenye kitoto kichanga.

mama huyo alipanda mpaka juu kabisa ya jengo lile lakini akashindwa kuruka na kichanga chake. basi ikabidi atafutwe golikipa mashuhuli ili kile kichanga kirushwe na kudakwa ili mama naye aweza kujiokoa.

jitihada zilifanywa huku moto ukizidi kusambaa kwenda ghorofa ya juu. basi akatafutwa gorikipa mmoja wa zamani (aliyekwisha staafu michezo)kwa jina na Owen, basi baada ya kipa huyo kuwa chini ya jengo liungualo, kikarushwa kile kichanga. kwa madaha, mbwe mbwe akakidaka kile kitoto.

kwa taifa kama uinegereza ni sifa sana kuokoa kiumbe ambacho ilibidi kife. basi kipa yule alijinyakulia sifa kwa kuokoa kichanga hicho

lakini ilikuwa hivi: mara baada ya kudaka kichanga hicho, umati uliokuwa pale ulishangilia vibaya sana, kutokana na kushangnilia huko, yule gorikipa wa zamani maarufu kama Owen, alijisahau na kudhania yuko uwonjani na hivyo kulejea enzi zake

alichokifanya ni kili kifanyacho na makipa wote baada ya kudaka mpira. yaani alikishika kichanga kile kama mpira, akakidunda chini na kukitwanga teke, kikafariki dunia. badala ya zawadi na kutuzwa akafunnguliwa kesi ya kuuwa!

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kamala duh! hii stori kwanza ilinifanya nifurahi lakini mwisaho nimelia, nimelia kabisaaaaa

SIMON KITURURU said...

DUH!

Upepo Mwanana said...

Maskini weeee

Candy1 said...

Mmh... :'(

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Kulia ni sawa! Lakini ni mara ngapi ktk maisha ya kawaida tunakuwa kama huyo KIPA? :-(

manake tunweza KUSHOBOKEA jambo mpaka ikawa nongwa na matokeo yake yajatuathiri siye wenyewe na wale wanaotuzunguka!

Imajini: Unamchukia Ng'wanambiti na kila apitapo wewe wanuiza mabaya yampate juu yake wakati wala yeye anaendelea KUNONA tu! Matokeo yake wewe unaendelea kukonda zaidi na unawaathiri wale ambao wanakusikia kwa kuwa nao wanajenga chuki dhidi ya mtu ambaye pengine ni mwema tu :-(

Aksante kamarade kamala!

mumyhery said...

ukumsifu mgema tembo hulitia maji