Monday, March 29, 2010

matokeo ya kili zetu.

nikubaliane na damija katika suala la tofauti za akili kunasa haraka, ila kuna ukweli juu ya chakula lakini hata mambo kama meditation yanasaidia sana akili yenye afya bora kuwa kali na kufanya mambo makubwa na ndio maana wahaya wanaonekana kuwa na akili

kwanza ni chakula bora, na mazingira. na ndio maana shule nyingi zilizojengwa vizuri mahala patulivu, zikifuatiwa na chakula na malazi bora hufanya vyema sana. hii hutokana na mazingira yaliyokaa ki-meditation. Seminaries

maiwaifu nikichwa (kutokana na matokeo yake shuleni) nilipomhoji aliniambia kuwa tangu darasa la kwanza mpaka form six alisoma kidogo, alipoenda kulala alikumbukia yote aliyoyasoma kabla ya kusinzia na asubuhi aliyakumbukia kwanza kabla ya kufanya lolote. hii ilimfanya kuwa nayo na kuyakumbukia milele. ni aina fulani ya meditation isababishwayo na chakula bora na mazingira mazuri na utulivu wa akili,

hata hivyo akili za wanadamu na hasa wadhungu wadaio waafrika hatuna akili japo wakerewe na wahaya wanazo, ni sumu, ni matatizo. mtu anatumia akili kutengeneza siraha za kuuwa wengine! anapewa tuzo. pamoja na akili ulimwengu umejaa maasi na wanajisifia kwa hilo, wanajisifia ukoloni nk

sasa dunia inawaka moto, tuko kwenye hatari za mafuriko, ukame, vimbunga, njaa nk, ni matokeo ya kazi za akili!!!!!!!!1


ila waliochanganya akili zao na ukweli / uhalisia / umilele / Umungu au umoja na sisi, walionekana machizi lakini kazi zao daima hazifutiki. namaanisha wale walioishi kiroho hata kwa kiasi kidogo kama vile Yethu Kristo, SAW, Budha na baadhi ya waafrika wasiojulikana kwa sababu za kikoloni

hawa akili zao zinaonekana na mpaka milele ni muhimu japo ni kama hazitusaidii lolote

ila sasa kuna wenye akili kama Nyerere, walifanya mengi lakini ujinga uliwafuata tu. eti unaweza kujiuliza kwa nini Nyerere aliivamia Uganda na kumng'oa Amin?eti kulinda mpaka wa kikoloni asiouweka, usiomhusu lakini leo tunaongelea jumuiya, tunaongelea kuvunja mipaka kutengeneza nchi moja, je Nyerere alikuwa na akili katika uvamizi wake????

4 comments:

Munale said...

Vp kuhusu akina Matondo na
wenyewe ni vichwa?

Mija Shija Sayi said...

@Munale, Kuna vitu hata si vya kuuliza mara mbili.
Chezea Matondo.

Tandasi said...

we likamala! kuhusu Nyerere umeenda chaka bovu alicho fanya nizaidi ya kulinda mipaka ya kijiografia yeye kama kiongozi wa eneo lake - taNGANYIKA ilikuwa ni kulinda usalama wa watu wake, kulinda uchumi wa nchi yake kutaja machache..ndio maana mataifa yenye nguvu mfano MAREKANI wanapenda kuona wanaitawala dunia lakini si yao ni ya MUNGU lakini dunia ni eneo wanaloishi hivyo wanalinda usalama wa maslahi yao na uchumi wao...SIUNGI WAZO LAKO KUWA UJINGA ULIMFATA NYERERE ila wajinga ndio...wali...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@tandasi, unaweza kuwa sahihi kwa mtizamo tu