Saturday, March 13, 2010

Matondo na IQ kubwa kwa wasio na dini, vegetarian nk

Nilishindwa kubandika maoni kwanye post iliyotundikwa katika blogu ya chakula kitamu, kichungu na kichachu, vyote vinaweza kumfanya mlaji kukuja (kama alikuwa hajakunja) au kukunjua (kama alikuwa kakunja) uso


Matondo anadai ya kwamba, watu wasio na dini wana akili kubwa, labda ni kweli au ni kwamba sio wavivu wa kufikiri. Hivi kwa nini huaminishwe? Lakini je kwanini dini zionekane kuongelea wakati ujao kuliko uliopo? Kwa nini zikemee tamaduni za wengine kwa jina la shetani? Kwa nini ziongelee shetani kuliko Mungu nk nk


Inabidi uwe mvivu wa kufikiri ili uaminishwe dini hizi tupelekwazo kwa lazima. Kwa mfano, mtwiba a.k.a kijana wa changamoto a.k.a mzee wa changamoto aliaminishwa kuwa tetemeko la ardhi kula Haiti ilikuwa ni adhabu kwa watu wasioamini Mungu wa wadhungu, eti wanaabudu dini za asili. Hii haiitaji kufikiri sana kukona kuwa anayesema haya ni mwendawazimu kwani waafrika na watu wengina wamekuwepo na wameishi miaka mingi bila kumtegemea Mungu au dini za kigeni mbona hakuna matetemeko au hawajafa?


Pia matetemeko na majanga mengine hayakuanza leo. Sasa eti yule mtu aliyakaa chini ya kifusi alisema kuna mtu mwenye mavazi meupe alikuwa akimletea maji na sio chakula, mtu huyo pia aliweza kumletea yule jamaa maji chini ya kifusi lakini akashindwa kumtoa pale!! Huu ni mfano tu wa jinsi y a kufikiri. Kutokukubali hadaa ni kuamua kufikiri mwenyewe badala ya kuacha wengine wakusaidie kufikiri na kukuaminisha na ndio maana ma-atheist wanaweza semwa kuwa na akili nyingi sana


Swala la uliberali nalo ni muhimu, wewe umekuja na kukuta mambo, kila unachokijua umemezeshwa, sasa iweje unakuwa mhafidhina? Kwa mfano kabila lako sio lako kwani hukuomba kuzaliwa pale, dini ulipewa wala hukuchagua, siasa ulizikuta nk, kwa nini usiwe mliberali badala ya uhafidhina wa usichokijua?? Mambo ya ushoga nayo wewe sema uko upande gani then kaa kimya, huna upande kama unafanya au unapenda ni wewe, kama hupendi sio wewe sasa je


Suala la u-vegeterian hapo ndo peeenye. Sasa iweje mtu ule tu vyakula hata kama huvihitaji mwilini mwako? Ehe ule mpaka sumu? Katika ulimwengu huu wenye misosi lukuki niyoharibu afya mtu ukiweza kubagua vyakula vya hovyo katika umri mdogo, lazima watu wakushangae wasioelewa, watakuona mjinga na chizi lakini wanaoelewa watukupongeza, kukushangaa na kukukubali au kukufuata katika hilo


Kwa hiyo ni kweli, tuna akili nyingi ila inaweza isiwe tofauti na wengine, ishi ni kwamba, tunafikiri wenyewe, hatumwachii chizi yeyote atusaidie katika kufikiri. Asante Matondo kwa utafiti huu

5 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

sijui mimi niko upande gani: wa vilaza ama wenye akili....lol

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Post hiyo inapatikana hapa:

http://matondo.blogspot.com/2010/03/utafiti-watu-wanaoamini-kwamba-hakuna.html

Huu siyo utafiti wangu - mimi na sayansi wapi na wapi? Huu ni utafiti wa watu na kama kawaida yangu, ninaposikia hizi tafiti za "ajabu ajabu", nazibandika kibarazani kwangu. Niliposoma "wanasifia" mavegetarian basi nikakukumbuka!

Mimi pia nimechoshwa na kula nyama na sasa nimehamia kwenye samaki ingawa nako sijui hawa wanatoka wapi. Tatizo la hapa Marekani ni kwamba hata kama ukihamia kwenye mboga nako ni yale yale kwani mboga hizo zimekuzwa kwa makemikali makali zaidi na zinaweza kuwa na madhara zaidi kuliko hata nyama. Juzi juzi hapa wamesema kwamba kuna kemikali fulani inayotumiwa sana katika ukuzaji wa mbogamboga ambayo imegunduliwa kwamba inawafanya vyura dume wawe majike na hawajajua ina madhara gani kwa binadamu. Mambo hayo.

Ukitaka kula mboga ambazo ni "organic" - ingawa huna uhakika kama kweli ni organic yaani zimekuzwa kiasili - bei yake itakutoa jasho kwani ni zaidi ya mara mbili ya zile zilizokuzwa kwa makemikali yanayogeuza vyura dume kuwa jike. Ni kuzungumkuti!

Yasinta Ngonyani said...

Hii habari itatufanya watu tusile kitu maana kila kitu ukila ...

SIMON KITURURU said...

Mmmh!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Chacha wewe si tuko kundi moja??
@matondo, mataifa yenu yaliyoendelea yana mikasa kibao, hata nyama ni za artificial, na mboga mboga sasa, na nadhani ndio chanzo cha makansa na magonjwa kibao.

ikitokea nikaenda kwenye sherehe naharusi, huwa nashangaa jinsi waTz wanavyokimbilia kutafuna makuku ya kisasa wakati angalau kuna nyama za kiasili zinazopaswa pia kuliwa kwa kiasi au kuepukwa

suala la mboga mboga za organic nk nalo linajitegemea. nilipokuwa Dar nilishuhudia mboga mboga kama vile nyanya, mchicha, spinach nk, zikimwagiliziwa maji yenye sumu za viwandani

kinachosadia angalau ukiwa huku utakula vyakula vibichi vya kiasiliviondoavyo sumu kali mwilini
binafsi sasa nataka kujikita katika kilimo cha matunda na mboga mboga

@yasinta sisi hatuishi ili tule ila tunakula ili tuishi kwa hiyo kula chakula kinachoishi zaidi (eat the living food)