Friday, March 19, 2010

mkoa wa kagera na maedeleo ya elimu


ni mkoa uliotoa wasomi weengi sana, lakini wenyewe ukiwa nyuma kielimu. mkoa hu ndo sasa utakuwa na chuo kikuu mwaka huu cha KKKT, kulikuweko na chuo kimoja tu cha ualimu yaani katoke. mkoa huu umekua na shule za kisasa maarufu kama english medium miaka ya 2000. zamani kulikuweko na shule za serikali, za dini kidogo na jumuiya mkao huu pamoja nakuwa na wasomi kibao, bado ulikuwa nyuma kwa kila kitu na sio elimu pekee.

waenyeji wa hapa wakirudi kutoka mijini hulewesha wanavijiji na kurudi. nilepoenda kwenye miji mikubwa kama Mwanza Arusha na Dar nilitarajia umoja na ushirikiano wa wenyeji wa hapa ili kuendeleza wenzetu na mkoa huu, nilishindwa nilipogundua kuwa wahaya wengi ni watu wa majigambo na pombe
yaani wewe ukitaka kuishi nao, nikulewa tu na kujisifia mkiwa baa,niliamua kuwatema marafiki zangu woote na hata wanandugu wa namna hiyo

na ndio maana mkoa wa kagera uko nyuma karibia katika kila kitu
nikiwa nahamia Bk niliwaaga baadhi ya wahaya waishio Dar kuwa mimi narudi bushi, walinishangaa na kunionya eti siwezi kuendelea kwani kuna wategemezi!! mimi nimelelewa na watu tu na kusaidiwa na watu, kwanini nami nisiwasaidie wengine?

je kuwasaidia wengine sio maendeleo? hapa ndo penya udhaifu wa wahaya, tunapenda tutajirike na kwatambia wenzetu badala ya kuwasadia woote yaani ndugu na wasio ndugu, wahaya na hata wasio wahaya
ndo maana mkoa huu uko nyuma

5 comments:

chib said...

Hapo umegusa sio karibu na ukweli bali ni kwenye ukweli hasa

Mzee wa Changamoto said...

Duh!!
Ndio twaitwa nshomile. TUNAJITAKIA HAYA YOTE KWA KUTENDA ULIYOSEMA.
Kama mhusika wa sehemu ya kinachotokea KAGERA na kama muathirika wa ninaloliona, nafanya KUTAFAKARI USEMALO na kisha kupanga namna ya kuendeleza jema nitendalo. Najua halitoshi lakini lazima lianzie mahala.
Tutafika tuuu japo twahitaji kubadilika saana.
PamoJAH

Mbele said...

Hii makala imenivutia. Wengine pia, ambao si waHaya, tunajipatia umaarufu kwa kutinga kijijini kwetu, kuwalewesha wanakijiji, na halafu kutokomea tena mjini au ughaibuni. Tuna jambo la kutafakari hapo.

Kuhusu suala la wa-Haya na majigambo napenda kuongezea kidogo hisia zangu.

Mimi ni mtafiti katika masuala ya masimulizi, tamaduni, fasihi na kadhalika. Na ninafahamu kuwa waHaya wana jadi ya masimulizi ambayo yamefungamana na majigamo. Kuna hizi zinazoitwa "enanga," kwa mfano, ambazo zinawahusu mashujaa kama akina Kilenzi (au Kachwenyanja), Mugasha, Rukiza, na kadhalika. Hayo masimulizi yamejengeka katika utamaduni wa waHaya, na pia makabila mengine ya jirani kama vile Uganda na Rwanda, na nchi nyingi za Afrika na dunia.

Kwa kutumia dhana hii, nahisi kuwa Mhaya anapokaa kaunta kwenye baa na kumwaga sera kuhusu yeye ni nani, anafuata nyayo za hayo majigambo ya asili.

Sijui ndugu Kamala una wazo gani kuhusu dhana hii? Ni hisia yangu, katika kujaribu kumwelewa huyu m-Haya anayemwaga sera baa, ili watu wamtambue yeye ni nani :-)

Anya said...

Hi Kamala
Have a wonderful sunday .. :-)

(@^.^@)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@ Mzee wa C?moto tupo pamoja katika ulisemalo

@ Prof Mbelle, inaonyesha ni kwa kiasi gani ulivyoiva katika masuala ya utamaduni kwa kuutaja utamaduni wa mHaya kiasi chake, nafikiri tamaduni za waHaya ni kati ya tamaduni za kijivunia sana kwani ni za aina yaka sena

kuhusu majigambo waHaya tuna majigambo mengi na labda kama ulivyosema ndio wanayojaribu kupeleka kila mahala hata yasipohitajika.

kwa mfano hata majina yetu, mimi naitwa Kamala--stabilizer, msuruhishaji nk Lutatinisibwa--asiyetishiwa walakuogofwa (nonfraightenable)na Lutabasibwa-- asiyewezekanika non-ebleable na vitu kama hivyo

na labda ndio maana waume wa kihaya huwa juu kwani majina yao mengi ni ya kibabe kama yakwangu na ya wanawake ni ya upole, unyenyekevu, urembo nk.

nyimbo zetu na simulizi zina mjigambo meengi mazuri sana ya kusifia utu wetu, uafrika wetu, uasili wetu, ardhi yetu na kufanya kazi kwa bidii, tabia njema na kadhalika. ila majigambo hay siku hizi yanatumiwa ndivyo sivyo na sisi kizazi kipya mpaka kero.

nadhani ndio maana inakuwa hivyo baa, kaunta na hata ofisini

majumbani mwetu akijamgeni huwa tunatambulishana kwa vigezo vya elimu na kazi mtu aifanyayo.

@Anya, thx