Monday, March 1, 2010

nini kimeliua jarida la kwanza jamii?

Gazeti la kwanza jamii lilianza kwa mikwara mizito kiasi kwamba watu kama akina Matondo wakawa wanapendekeza vitu kibao juu ya ni vipi liweze kusomeka kwa walio wengi,

jarida hili sasa halipo mitaani tena, kwa kile ambacho mmiliki na mwendeshaji wake alinielezea kuwa ni kukosekana kwa wateja.

binafsi niliishaona jinsi litakavyokufa kwani liliiga magazeti mengine., gazeti hili pamoja na kwamba lilikuwa na nafasi kubwa ya kuja kwa mmtindo mpya na unaopendwa na waliowengi, liliiga magazeti yaliyotangulia ya udaku wa kisiasa.

hivyo lilipendelea kuandika habari za mshutusho (shocking news) badala ya kuja na vitu vingine vya tafauti vinavyopendwa kama utambuzi, mada za bloguni, teknolojia, utamaduni, nk

lilijikita kuandika habari za uongo na kweli (kama yalivyomagazeti mengine ya Tanzania) badala ya ishu muhimu. Jambo hili lilipelekea kukosekana kwa wasomaji wengi kwani waliishazoea vichwa vya habari visivyokuwa na maana kwenye magazeti mengine

pia lilijikiti kutumia waandishi wenye majina makubwa kama maprof, na watanzania waishio ughaibuni ambao hoja zao mara nyingi ni za kitaalamu zisizoeleweka sana kwa waTZ wasiosoma.
nikiwa mwandishi kuna wakati makala zangu zilichelewa sana kutoka au zisitoke. katika halia ya kujiuliza tufanyeje, mwendeshaji wa gazeti hilo alinitafuta nami nikampatia ushauri ambao kama angeufuata basi gazeti hilo lingependwa sana tanzania

l;akini kwa kuishi kwa mazoea na labda kutojiamini, gazeti liliendelea kuwa na vichwa vya habari za kisiasa uchwara japo mmiliki mwenyewe alikiri kuwa wasomaji walimpigia simu wakidai gazeti hilo limependeza baada ya kuongeza makala za utambuzi na vitu vingine vya kitanzania.

kuonyesha kuwa hakuna matumaini, sasammiliki wa gazeti hilo anaandika makala katika gazeti la Raia Mwema na hivyo yawezekana limekufa kifo cha Mende

Somo,; Tuache kuiga, tutafute vitu vipya na vya kwetu

6 comments:

Tandasi said...

labda utafutaji wa masoko kihabari ulikuwa mdogo, labda gharama za uendeshaji zilikuwa kubwa, labda labda mada zilikuwa kitaaalamu na zilitesa watu wasiopenda andika ya kisomi kwangu mi ni labda tu. lakini mwanahalisi, raia mwema ni wale wale mbona wapo?. sijui.

Fadhy Mtanga said...

Kaka Kamala sikuwa aware kuwa Kwanza Jamii hatunalo tena.
Nakumbuka nami nilijitosa kutuma mashairi mule ingawa habari za siasa na vitu kama hivyo viliyakosesha nafasi. Lakini nililipenda sana.
Anyway, pengine wanajipanga ili waje na mshindo mkuu.

Munale said...

Maggid aliniambia kuwa gharama za uendeshaji zilikuwa kubwa kutokana na
kukosekana kwa matangazo ya
biashara pia,anyway ninampongeza kwa kuthubutu
kuanzisha gazeti na napenda
kumshauri kwamba ajipange
vizuri ili alirudishe mitaani gazeti hili kwa
sura mpya

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Tazama pia maoni yaliyotolewa na wadau kuhusu suala hili hapa:

http://matondo.blogspot.com/2009/12/gazeti-la-kwanza-jamii-sasa-kuchapishwa.html

Mimi nadhani gazeti hili halikuwa na ajenda na dira (sahihi). Lilionekana kama lilikuwa linatangatanga huku na huko kati ya Raia Mwema, Rai na Mwanahalisi. Makala za kitaalamu za maprofesa pengine halikuwa jambo baya kama zingetengewa kurasa chache na kurasa zilizobakia zikajikita katika lengo hasa la gazeti. Mojawapo ya ushauri wangu na wanablogu wengine ilikuwa ni kujaribu kutenga kurasa angalau mbili au mmoja tu kwa ajili ya mambo moto moto kutoka kwenye blogu, masuala muhimu kutoka vijijini na ukurasa maalumu kwa ajili ya wanafunzi mashuleni.

Na kwa mazingira ya sasa, makala za utambuzi zinahitajika sana na ukurasa mmoja maalumu ungetengwa kwa jambo hili. Mtu mwenye ukurasa wa kudumu kama Kamala ingebidi alipwe kwa kazi hii ili aweze kuandika makala kila Juma.

Ninavyojua mimi ni kwamba wachangia mada karibu wote walikuwa wanaandika mada zao bure na walikuwa hawalipwi cho chote. Huu ulikuwa ni mchango wao kwa jamii. Kwa hivyo inashangaza na kusikitisha kuona kwamba pamoja na kujitolea kwa waandishi mashuhuri kama Padri Karugendo, Joseph Mihangwa, Profesa Mbele na Profesa Born Again Pagan na wengineo bado tu gazeti hili halikunusurika.

Naandika makala kuhusu mchango wa magazeti ya Udaku na kupendwa kwake na nitaligusia swala hili.

chib said...

Wasomaji wa magazeti pia wamepungua, nafikiri watu wengi hawana utamaduni wa kupenda kusoma kwa ujumla. Kuna watu wameanzisha biashara ya kulipa nusu ya gharama ya gazeti na kupewa dakika 10 za kusoma halafu wanaliacha gazeti papo hapo likisubiri mteja mwingine.
Wasomaji tunapaswa kuchangia sekta hii ya magazeti kwa kununua na kwenda kusoma

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@tandasi, nadhani umejibiwa na matondo, @mtango, ni changamoto kubwa kukosa nafasi kwani liliihs kwa mazowea

@munale, nikweli gharama zilikuwa kubwa na katika jambo lolote gharama huwa zipo ila ilikusekana mikakai madhubuti ya kukabiliana nazo kama kuja na vitu vya tofauti kama asemavyo matondo ili wasomaji wawe wengi na watangazaji wazaliwe

@matono, maoni yako yanaonyesha vitu muhimu vilivyokosekana katika gazeti hilo na hivyo likawa halieleweki, ishu za vijijini, utambuzi, usomi makini nk, vingelifanya kuwa la tofauti na la kijamii zaidi na hivo kuyashinda yoote yaliyoko sokoni!!!! ni kweli hii, tuanzishe la kwetu nini??

@chib, kinachopunuza wasomaji ni porojo na propaganda za kwenye magazeti, llikiwa makini watanunua tu!