Friday, March 5, 2010

safari hiyo tena wandugu


baada ya safari na matembezi ya majuma mawili nanusu, sasa Jmosi ni wakati mwingine wa kupanda basi kuleekea kwetu mikoani kanda ya ziwa kujiunga tena a familia yangu niliyoimiss saana na shughuli za kiofisi vile. najisikia furaha kurudi home lakini zaidi kukutana na maiwaifu ambaye nilimkosa (miss) vyakutosha. nitakuwa kimya kwa siku mbili tatu kwani mapumziko ya kutosha ni lazima

5 comments:

Munale said...

Nakutakia safari njema
Kamala na mapumziko mema!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Safiri salama na mapumziko mema.....

Halafu sijui kwa nini nakereketwa sana kuweka "kwesheni maka" mbele ya haya maneno yako "nitakuwa kimya kwa siku mbili tatu kwani mapumziko ya kutosha ni lazima"

Tandasi said...

hah hah Profesa matondo hunifurahisha siku zote kwa uchokozi wake SAFARI NJEMA KAMALA BWANA wa MAJESHI akushikamanishe na mema akuepushe na vibaka wa njiani

Yasinta Ngonyani said...

Usafiri salama na uwe na wakati mzuri.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@munale, shukrani, na nitakuwa Musoma mwezi huu tutawasiliana

@matondo, sioni haja ya kwesheni maka, kwani wewe hujawahi kuwa mbali na maiwife wako then ukarudi?? unakuwagaje?