Tuesday, March 9, 2010

strange facts in Bukoba!


Bukoba ni mji pekee ambao huruhusiwi kuendesha gari lenye vioo vyusi (tinted). ukikamatwa unapelekwa cetral police, unalipa faini na kuvibandua huko! nilishangaa kwa nini sioni magari tinted hapa

bukoba pia ni mji pekee ambao ukiwa na mahitaji ya dukani saa saba mchana, ukafilie mbali na hela yako. wahindi na wafanyabiashara wengi wa mji huu ni waisilamu na hivyo saa saba ni muda wa swala, wewe, utajuuuuuta kuwa na mahitaji muda huo

lakini bukoba ni mji pekee unaouza juisi ya nanasi na embe kwenye chupa kama za soda, juisi hiyo maarufu kama 'mali juisi' haina kemikali yoyote, unaweza kuinywa wakati wowote iwe kwenye jokofu au isiwe huko, ladha na ubora n i ule ule
wewe, Nyegera waitu (kaaribu bwana)

8 comments:

Tandasi said...

bukoba na mambo yao!

chib said...

Hiyo juisi inatengenezwaje mkuu. Kuna ile ya ndizi a.k.a mlamba ni tanu sana, lakini inavyofinyangwa kwenye majani wakati inatengenezwa, Duh!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@Chib, juisi ie naona kuna kiwanda kinataengeneza. mlamba ni bomba tatizo hualalagi kwamba ukiutengeneza leo lazima uunywe wote vinginevyo unachacha

SIMON KITURURU said...

Bukoba ni moja ya sehemu ambayo sijawahi kufika.

Ila kwa kuwa nimeguswa kidogo na MADUKA kufungwa saa za swala ,....

.... naweza kusema Tanzania kuna sehemu mahitaji fulani huathiriwa sana na DINI. Na naweza kukiri ukiondoa WAISLAMu Tanzania kuna sehemu nyingi hasa za starehe unaua biashara zote kwa kuwa waendeshaji na wateja wengi wa msingi ni waislamu.

Kwamfano hata MWANZA MJINI last time nilipokuwa pale mahitaji yangu ya KILAJI yaliathiriwa sana na kuwa ilikuwa MFUNGO ramadhani kwahiyo sehemu kibao ambazo zinatibu mahitaji yangu zilikuwa zinafungwa, na silizo wazi wateja wakuhesabu .

:-(

Hivo juisi kwanini hazisambai Tanzania nzima?

Bennet said...

Alikeni wachaga wajekufungua maduka, hata akiwa muislam duka atafungua asubuhi mpaka jioni

Anonymous said...

Naukumbuka mji wa Bukoba....
kufuatia kundi la wapigania uhuru wa Uganda kuvuka mpaka na kushindwa...mwaka 1972!

JKT kutoka Ruvu, Makutupora (Dodoma), Bulombora (Kigoma) na Ol-Joro (Arusha) tuliletwa hapo Kambi ya JKT Kaboya kusaidia ulinzi - viongozi wakombozi wa Uganda wengine walikuwa wameweka kambi yao hapo.

Ilikuwa ni wakati mgumu sana hapo kambini Kaboya. Tulipigwa na mvua kubwa na ubaridi wa usiku na huku tukilala mhandakini na kupikia msituni.

Baada ya juma moja hivi, baadhi yetu tulisambaza hapo mjini kulinda majengo ya serikali, benki na vituo vya mafuta.

Tkiwa hapo kambini kaboya na hata hapo mjini Bukoba, tuliweza kujipenyeza kufurahia ukarimu wa Kihaya kwa kunywa "lubisi" kwa wingi na kumung'unya "akamwanyi".

Oh, Bukoba, sitasahau Hamugembe na Bukoba Coffee Tree!

BAP

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@simon, sijui kwa nini isisambae
@bennet, wachaga wapo ila wachache, ukienda sehemu usikute mchaga basi ujue hakufai kuishi

@BAP. nikipata kamera ntakutundikia picha zote za maeneo uliyoyataja. ila kaboya naogopa jeshi

Anya said...

Looks like a wonderful place :-)

(@^.^@)