Saturday, March 27, 2010

swala la kuwa na akili na kutokuwa nazo

kuna mjadala mzito saana juu ya kuwa na akili, bila shaka kamakuna akili basi kuna kutokuwa nba akili pia. bado najiuliza sana juu ya jambo hili japo kila mtu anamawazo yake. ila hakuna anayejisema kama ana akili isipokuwa mimi tu ndo nafanya hivyo
tunajiuliza mwenye akili yukoje, lakini hakuna anayejilejea, sasa mwenye akili ni nani? au sisi sote ni wajinga (hatuna akili)? sasa je tusemeje kwa hili?
kuna wanaohusisha akili na rasilimali, utajiri au umasikini ila kuna masikini wasiopenda kutajirika. kwa mfano mzee mmoja alikuwa navua samaki wawili kila siku. mmoja anamuuza kupata fedha na mwingine ni kitoweo nyumbani. bwana mmoja akamshauri avue samaki wengi na kuuza badala ya wawili tu kwa siku.
yule mzee akamuuliza ili iweje? jamaa akasema, utafika hatua utamiliki boat kibao na mameli ya uvuvi, ili iweje? akauliza, utamiliki viwanda vya sama na kuuza samaka nje ya nchi, ili iweje? akauliza, utaajili wafanyakazi wa kukuingizia pesa harafu utakuwa na Muda wa kukaa na familia yako. mzee akamwambia yule bwana kuwa ndicho akifanyacho sasa, yaani kukaa na familia yake
kwa macho ya nche, zee hili ni fala, lakini kwa jicho la Ndani je??
wabongo wanahamia miji mikubwa na kuruka majuu yaani ulaya/amerika kama mzee wa Changamoto, lakini baadhi kama mimi tumehamia mikoani tena vijijini, hatuna akili sio ehe???
suala hili bado ni pana, akili zinahusishwa na tamaa ya binadamu ya kutaka kumiliki dunia, kutaka kumiliki ulimwengu huu na kutaka kujifanya kama hajui kuwa yeye siye wa ulimwengu huu
watu wanakushangaa kwa kula chakula bora na Muhimu mwilini (vegeterian) huku wakiona matatizo lukuki yaletwayo na kula hovyo! wanaema huna akili wala hufurahii maisha, are they shuwa?
watu wanaaminisha vitu vya kijinga eti wana akili, hawafikirii, wanasaidiwa kufikiri nk nk. ila hata mimi ni mjinga japo nina akili. bila kiasi cha ujinga ni hatari. mambo mengi niyafanyayo ni ya kijinga japo nina akili (naomba nisiyatolee mfano hayo)
suala la akili!!!

3 comments:

NuruShabani said...

Mi nadhani kila mtu anazo akili zake.Isipokuwa jamii imeaamua kuziweka katika makundi,kuna wale ambao wanaonekana wana akili na wasio na akili.Ukichunguza utaona hakuna aliye kamilika, unaweza ukawa ni mzuri sana katika masomo ya darasani lakini ukawa haujui kucheza mpira.Kwa mtazamo wangu watu wote tuna akili.

Mija Shija Sayi said...

Kamala hii ya mkeo ni kali. Nimeipenda sana mbinu yake nami naomba nimuazime. Halafu inaonekana wewe ni mtaalamu wa Meditation ukipata muda tupe somo basi na sisi tufaidike labda itasaidia kututuliza akili.

@Nuru Shabani, baada ya kusoma komenti yako nimejikuta najiuliza kama kuna tofauti ya akili na kipaji.

Kamala hii nayo tupandishie siku moja kibarazani tuchambue kwa undani tofauti ya akili na kipaji kama zipo.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@damija, ni kweli inabidi tuifanyie kazi juu ya akili na kipaji, sidhani kama mimi ni mtaalamu wa meditation ila ni mpenzi wake, ni chakula changu cha kila siku, naihusudu sana kwa kweliinaendna na akili kuwa fresh

hiyo dhana ya mke wangu hata wataalamu wanairecommend, msisitize mwanao au hata wewe na utaona matokeo yake, ni noma

soma la meditatio nimewahi litoa kwenye mada za nyuma ila halijaisha, so nitalifanyia kazi