Monday, March 22, 2010

tatizo la dini za kukodi

Natamani kwenda Yerusalemu,

Natamani kwenda Yerusalemu,

Natamani kwenda Yerusalemuuuuu

Haleluya Yerusalemu

Hili ni mojawapo ya Nyimbo, a.k.a pambio tulizoimbishwaga tukiwa watoto. Mimi nilidhani Yerusalemu iko mbinguni au nineno mbadala la ahera, ila nilipokuwa mkubwa, nikaanza kusoma vitabu na kusikiliza habari, nilishangaa kwa nini nitamanishwe kwenda yerusalemu.

Kumbe ni mji wa vita na umwagaiji damu usiokuwa wa kawaida. Ubaguzi wa rangi, dini na kila aina. Harafu eti natamanishwa na mimi niende huko, kufanya nini?

Jamani wenye watoto tuwalee kwa uelewa sio kuwatamanisha kuacha nchi yenye amani na kutamani kwenda kwenye kila aina ya machafuko. Tamaa kama hizi ni kumkosea Mungu aliyetuleta kwenye Amani.

Sitamani kwenda Yerusalemu X3

Haleluya Tanzania

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Amina!!

Tandasi said...

milele Tanzania!

Mija Shija Sayi said...

Kamala kakangu hii bambio umeitizamia jicho gani?

Anonymous said...

@Da mija: Kaitizamia jicho la nje huyo!!!

chib said...

:-)

SIMON KITURURU said...

:-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@damija, swali lako ni la msingi saana kwani inafuatana hiyo Yerusalemu inawakilishanini, na ni mtizamo zaidi kuliko uhalisia, si unajua misahafu a.k.a Biblia n itafsiri zaidi kuliko ilivyo? kwa hiyo tafsiri ya mtu inamata zaidi hapa

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kamala, pengine itabidi tumtume Mchungaji Kakobe aje "akulokoleshe" Unasemaje?

Born 2 Suffer said...

Tanzania oyeee.