Thursday, March 4, 2010

wanadamu na kupenda kula nyama

Wanadamu tunapenda kula vitu kibao hata kama havina umuhimu wowote mwili zaidi ya kuwa sumu. Nikiongea na rafiki yangu mmoja aliyeniuliza kwa nini siri nyama, alishangaa sana swali nililomuuliza. Baada ya kumpa majibu kadhaa nikamuulia kama aliwahi kusikia daktari akitoa pendekezo kwa mgonjwa yeyote kuwa ale nyama kwa wingiiiii!! Jamaa alicheka na kuuona ukweli uliomo humo. Eti wewe umewahi sikia hiyo daktari akimwambia mgonjwa kula nyama kwa wingi au kunywa soda nyiingi sana?? Si utaambiwa madhiwa (maziwa), kula mboga za majani nk?? Sasa kwa nini usubiri dakari aseme? Unapenda sana ladha za midomoni ehe???

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala hivi kwa nini wewe huli nyama. Sasa mbona nitapata taabu sana utakapofika huku itabidi nipika vyakula aina mbili duh! kazi kwelikweli!!!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Da Yasinta: huna haja ya kuwa na wasiwasi kwa kuwa anaweza kukaa akakuangali ukila ulichopika....lol

Natumai atapata manyasi a.k.a salad ambayo nadhani itamtosha...lol

au vp Kamala?

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Nanukuu....

"I did not climb to the top of the animal kingdom ladder to eat grass!"
Mwisho wa kunukuu.

Hili lilikuwa ni jibu lililotolewa na jamaa mmoja (comedian) alipoulizwa ni kwa nini alikuwa anapenda sana kula nyama.

Linasadifu ama?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@Yasinta, niliisha sema sana katika makala zilizopita kwa nini siri nyama, hata hapa nimesema ya kuwa Nyama sio chakula muhimu kwetu kisayansi na Kiroho sio chakula kabisaaaaaaa

@Chacha, you are right natumai kuna kachumbari, salad, matunda nk huko sweden. angalizo kwa yasinta ni kwamba situmii vilevi!! mgeni gani huyooo

@matondo, animal kingdom?? maanake nini kwani binadamu sio mnyama? je anasemaje kwa wanyama wasiokula majani? je ni kweli huyo jamaa hali majani?? eti anaishi kwa kula tuu nyama bila mboga mboga a.k,a majani nk?

chib said...

Tafsiri mbaya ya ulaji wa nyama inaweza kufanya ukaichukia.
Nafahamu kula nyama kwa wingi sana kunaweza kukuletea madhara hasa katika mfumo wa damu, tofauti na ukila jamii ya mimea ambayo unaweza kula utakavyo.
Wazungu hushauriwa kula kiasi au kuacha kama wako kwenye hatari ya kupata magonjwa ya moyo hasa cholesterol inapozidi, na kuna watu ambao wanapata matatizo hayo kifamilia zaidi.
Waafrika wengi ambao wanafanya kazi na kutembea sana hawako katika hatari ya kudhurika na nyama kama wale wanaotembea wakiwa wamekaa, yaani gari - ofisini tena kakaa halafu gari kwenda nyumbani.
Wamasai chakula cha kila siku ni nyama maisha yao yote, lakini hawana matatizo ya kama watu wanaopenda kukaa tu.
Mie nyama nakula, lakini najua kiasi changu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@chib, angalau unajua kiasi chako. baadayenitaongeleavizuizi vya kula Nyama kiroho

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Inawezekana huyu jamaa nilimnukuu vibaya. Inapaswa kusomeka hivi:

"I did not climb to the top of the food chain ladder to eat grass!"

Sijui kama inatofautiana na ile nukuu ya mwanzo.