Thursday, April 29, 2010

katika kub adili misemo ya zamani kuwa mipya

kuna kizazi kipya, cha dotcom au cha kwetu, kuna cha iPod na sasa iPad na vinginevyo. ukizeeka, unapitwa na wakati, nikweli kwamba kuna vitu au lugha za kizazi kipya huwezi kuzielewa na utaihia kuwa tukana na kuwaepuka, sasa tuangalie baadhi ya misemo ilivyoboreshwa ili kukidhi mahitaji ya kizazi cha leo,

asiye a mwana, hajazaa

simba mwenda pole, hana haraka

aliyeko juu, mpandie huko huko

asiyesikia la mkuu, ni kiziwi

ukiona vyaelea, si vizito (vyepesi)

ngoja ngoja, huleta njaa

mwenye macho, si kipofu

kama unafahamu misemo mingine iliyoboreshwa ili kuendana na kizazi chetu, karibu tushirikishane

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Wow! kwa mimi hiyo misemo ni kweli mipya kabisa kwani kila nikifika nhyumbni au soma kitu nakutana na mapya. kwa kweli itabidi nije nyumbani kila mwezi...LOL Asante Kamala nitaprint ili nijifunze nsije umbuka nkija huko.UPENDO DAIMA

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Da Yasinta: kwa kweli UTAUMBUKA kwa kuwa ukijibu kama alivojibu Kamala watakucheka WATU!!!!

Kalagabaho....lol

Fadhy Mtanga said...

Ndiyo maana kizazi cha sasa unatakiwa kuwa makini unapotaka kuongea neno. Siku moja darasani mwalimu wetu wa hesabu (wa kizazi cha mwalimu) akizungumza na kizazi chetu, akasema "watu wengi hesabu zinawachenga"
Darasa zima likalipuka kwa kicheko. Sijui kama alielewa kwanini twacheka.

Anonymous said...

Ukitaka kuona cha uvunguni, sharti unyanyue kitanda!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@fath namimi sijui

@anony, au atambae

Anonymous said...

Ana ana do kachanika bastoo ispiring matingooo kalamba mchuzi unanoga tena sana sana kabisaa