Friday, April 9, 2010

nimtolewa nje benk ya NBC tawi la Bukoba


nikiwa nimeamka mapema kuwahi foleni za kila siku za benki, nimekutana na kuubwa leo baada ya kutolewa nje ya Benki hiyo kwa kosa la kuongea na simu na kusoma SMS ndani ya Benki hiyo tawi la Bukoba tumeingia tukiwa wengi ndani ya benki hiyo, na baada ya kufika ndani tukaambiwa benki hiyo haina mtandao hivyo ni vigumu kufanya transactions zetu.

nikaamua kumpigia simu mdogo wangu niliyekuwa namtumie pesa za shule kama anajinsi, anitumie namba ya Acc katika benki nyinginezo ndipo akatokea mlimzi aliyevalia mavazi ya bluu na kuniambia kuwa nisiongee na simu nikiwa ndani ya benk yake nami nikamueleza kuwa mteja ni mfalme. mlinzi huyo akasimama mlangoni akiniangalia kwa makini hukuakiniahidi kuwa nitaona.

nikaamua kuitoa simu yangu mfukoni ili niizime, ghafla akaja askari mwenye Bunduki aliyevalia mavazi ya kikosi cha kutuliza ghasia FFU na kuniambia nitoke nje, akaniambia kanifukuza kwa leo ni niondoke, sikumwelewa. akaanza kuniambia kuwa niondoke, nami nikataka nimwone mtu anayehusika na huduma kwa wateja katika benki hiyo ili nimwelize shida yangu na yeye anieleza juu ya taratibu hizo, mlinzi huyo akakataa na kuniamuru niondoke.

Benki hi nimekuwa nikikutana na vikwazo visivyo vya kuwaida na labda ndio taratibu zao. majuzi nikiwa namtumia mdogo wangu ela, nilisahau kuandika namba ya mwisho ya akauti yake, mdada aliyenihudumia alinifukuzia mbali na kufuta (cancel) form zangu kwamba nisimsumbue, kuangalia vizuri ndo nikagundua kuwa kuna namba inakosekana. nikajaza form nyingine na kumpa akaingiza mhamala ule, yaani alishindwa kuniambia juu ya kukosea kwangu kwa kusahau namba moja wapo ambaye ningeijaza na na kumalizia mhamala ule

pia niliwahi kuingia benki hiyo kwa lengo la kuulizia taratibu na kanuni za kufungua akaunti ya kampuni, mwanadada aliyekuwa kwenye dawati la maulizo aliniambia yuko bize na hivyo nirudi baadaye, nikamuuliza kama yeye yuko bize hakuna mwingine wa kunisaidia?? akaniambia nirudi tu baadaye.

niliporudi majira yamchana akaniambia yuko bize bado ila akaniambia kuna mambo mengi ya kufanya likiwemo kwenda kwa mwanasheria nk, mimi nikamsihi aniambie tu taratibu zote, akaniambia nirudi tu baadaye

nilipopata safariya kwenda jijini Dar es salaam na kwenda katika tawi lao la posta (bila shaka ndo makao makuu ya benki hiyo) ilinichukua muda ya dakika kama mbili tu kupewa maelezo yale abayo ni rahisi tu kuelezeka na kufuatwa, nilishangaa nikabakia na swali kwamba nikifungua akaunti hiyo tawi la Bukoba nitaiendeshaje?

sasa kama kusoma SMS ni kosa ndani ya benki tutafanyaje katika Benk hizi za kisasa zinazokushauri kufanya baadhi ya mihamala kwa njia ya SMS, internet na hata ATM? je, kama namba ya akaunti ya yule ninayemtumia iko kwenye simu ni kosa kuifungua na kuisoma ili niiandika kwa usahihi?? je Benki zenye foleni ndefu na za kukaa muda mrefu ukisubilia huduma, inakuwaje usiomgee na simu kwa lengo la kuweka mambo sawa ofisini kwako au nyumbani au hata kama unasubiliwa na mgonjwa hospitali ili ulete pesa apate vipimo?

lakini je, mimi kama mteja, kwa nini nisiruhusiwe kuonana na mhusika wa huduma kwa wateja ambaye kimsingi yupo kwa ajili yangu???

leo nimekutana nalo hilo benk ya NBC tawi la Bukoba

6 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mbona mambo ya kawaida hayo? Mwaka 2007 nilikuwa najaribu kumfungulia Bwana mdogo mmoja akaunti pale Benki ya Posta makao makuu Dar es salaam. Mbona cha moto nilikiona? Tuliambiwa tukalete barua ya mkuu wa kitongoji. Nilipoulizia kuhusu masharti yote ya kufuata ili nikirudi tena maombi yale yawe kamili kamili mwanadada aliniangalia kwa jicho la dharau na kunisukumizia karatasi zangu. Halafu akaita mteja mwingine. Yaani iilikuwa kama vile nilikuwa naomba pesa kumbe nina pesa zangu mwenyewe na nataka kuziweka katika benki yao!

Customer service yetu bado ni mbovu hasa katika vyombo vinavyomilikiwa na serikali. Hata ukienda kununua tiketi ya ndege Air Tanzania nako utaangaliwa umevaa nini na huduma utakayoipata ni ya kijeshijeshi tu. Bado safari yetu ni ndefu katika hili.

Safari nyingine jaribu kulamba pamba za uhakika halafu uone mambo yatakuwaje. Huduma pengine zitabadilika. Mimi nilitupiwa karatasi zangu pale Posta nilikuwa nimevaa kaptula na kandambili tena ndiyo tu nimeshuka kwenye daladala!
Niliporudi tena nikiwa nimetinga pamba za kufa mtu, huduma ilikuwa afadhali kidogo na akina dada hata waliweza kunitupia matabasamu...

Kamala, safari nyingine wapige darasa la kujitambua tu hao halafu achana nao!

Yasinta Ngonyani said...

POLE SANA

Fadhy Mtanga said...

Suala la simu, benki nyingi hapa jijini zinakutaka uzime simu ukiwa ndani ya benki.

Suala la huduma mbovu wacha kabisa. Mwaka 2006 nilitaka kufungua akaunti na benki yako hiyohiyo enibisii. Majibu niliyopewa na wahudumu wake yalinifanya nisitamani tena kufungua akaunti kwao.

Wahudumu wa benki hawana majibu mazuri kabisa kabisa.

Wanasahau kuwa bila pesa zetu wasingekuwa na sababu ya kufanya kazi benki.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@matondo. mi kweli wanahitaji elimu hiy, lakini je wako tayari?? wao wanajiopna wanajua zaidi. na hasa hii ikoa ya mbali wao wanadhani kila mtu hajui tratibu zozote wala nini, wanadhani sisi sote ni mbumbumbu fulani.

kumbe tumewahi kufanya kazi kamahizo na kuamua kuziacha.

very interesting

nikiwa naondoka pale askari alijaribu kuongea maneno ya dhihaka ili labda nimtukane au nini sijui, nikamwabia haya ni maisha, yeye ana bunduki na uniform, akini ajue na mimi nina ofisi yangu ambayo naye atakuja tu siku moja kutafuta huduma na sitomlipizia wala nini

harafu kurushiwa matusi, niliwaangalia tu hao maaskari kwani wao wanalinda pesa, mimi naweka na kutoa pesa, sasa mkubwa ni nani jap kimaumbile sote tu sawa tu???

kwa upande mwingine, kujitambua ni muhimu tu sana

John Mwaipopo said...

@ prof matondo kumbe kiswahili cha uswazi nawe umo. hapana shaka kwa kuwa uko ndani ya fani.

kamala na fadhy haya madhila yoote yanatokana na upumbavu na tabia ya kutojitqambua.

waendesha benki wa tanzania wanasahau kuwa noti wanazozihesabu zimewekwa na akina sisi tunaopewa maneno machafu. Au kwao pesa ni ziel zilizowekwa na mafisadi? za kwetu zinawapa mafua.

tofauti na nchi za magharibi ambako huduma ya kawaida ya kibenki haichukui hata dk 10, hapa tanzania banki zilizo nyingi (ambako sie akina pangu pakavu 'hupitishia mishahara') zimeshindwa kumudu idadi ya wateja wao. promosheni yao haiendani na upanuzi wa huduma. mathalani benki hii ambayo mshaijua, foleni zake ni balaa karibu wakati wote wa mchana. ukitaka kwenda kutumia kaunta au ATM jiandae kukorofishana na mwajiri wako. ukiwahi sana masaa 6 yanakuishia kwenye foleni ama ya dirishani ama kwenye ATM. hivi unawezaje kukaa masaa matatu huku umezima simu katika ulimwengu wa sasa? wamekuwa na wateja wengi pasi na kuhakikisha uwingi huo uwe sambamba na ubora wa huduma. ndio maaana awali walikuwa sahii na wawazi tu kujiita 'ni zaidi ya benki', maana hapo ni gym, kijiwe cha story, ulingo wa porojo na mara kadhaa wateja wamekuwa wakianguka wakiwa kwenye foleni. nadhani sasa waweke First Aid Services.

benki zilizo nyingi ni hivi hivi. it's as if we've been forced to use their services. tumbafu! pia naomba niulize hivi chama cha walaji tanzania kinashughulika na nini kama sio kero kama hizi.

hao wa bukoba nadhani koero mkundi awaombee maana yao ni shida ya kwenda shule bila kuelimika. hao maaskari tuwaonee huruma tu maana khawajapambana na majambazi siku nyingi sasa wanadhani kila mtu ni jambazi.

John Mwaipopo said...
This comment has been removed by the author.