Tuesday, April 6, 2010

umuhimu wa kupumua!!!

wanaoitwa wataalamu a.k.a wanabaiolijia kama chi wanatuoya kuwa kuna aina kibao sijui za kupumua. nizifahamuzo ni pamoja na kupitia puani, vinyweleo na hata kujamba

sasa leo tuogelee umuhimu wa kupumua. suala hili ni kama sio muhimu kwani wengi hudhania hawapumui. katika maisha kuna mambo ya ajabu. ule uwezo wako wa kupumua ukikuondokea, watu wanasema kafariki. je hii ina maana kuwa sisi ni pumzi? kama sio kwanini ikikosekana twafa???

kupumua ni muhimu sana na labda ndio sisi wenyewe. kuna aina za meditation za pumzi za kuwaida na kuna nyingine huitwa pranayama nk. tukiwa kwenye nyakati ngumu huwa tunaambiwa kuwa "take a deap breath" nk ili tuwe sawa.

basi kumbe kupumua ni kitu muhimu sana na labda kuliko hata chakula katika maisha yetu. kupumua ni kutamu sana dugu zangu. kwa wale wanaopenda kujifunza meditation waweza kuanza na zoezi la pumzi, yaani kupumua ukiwa umekaa wima (umenyoosha mgongo) au ukiwa umelala chali na kwa kunyooka. waweza kulala chini (sakafuni) au ukalalia mkeka au godolo jembamba.

basi anza kuingiza pumzi ndani taratibu na kuzitoa taratibu pia. fanya kwa muda kama nusu saa hivi. wakati unafanya zoezi hili hakikisha huna mawazo zaidi ya kuiwazia pumzi. ukiingiza ndani ione inavyoingia na ukiitoa ione inavyotoka. isikilizia inavyopita katika kila kiungo cha mwili wako. ukimaliza zoezi hili usikurupuke kuinuka juu. relax kwanza hapo ulipo, jiambie sasa utainuka, tulia kama dakika tano ndo uinuke. kuinuka ghafla kwaweza kukuletea matatizo

hapo utaona umuhimu wa pumzi maishani mwako, jisnsi inavyofanya makuu. jiulize ukienda bich au sehemu isiyo na watu kwa nini huwa unajisikia fresh na kuingiza pumzi nyingi?? nk nk

pumzi ni dili sana wandugu

1 comment:

Tandasi said...

pumzi ni sawa na mafuta kwenye pikipiki unapoiwekea mafuta ndivyo iavyokuwa nyepesi kuendesha!