Monday, April 19, 2010

wagombea ubunge jinbo la nkenge

nipo latika jimbo la nkenge wilayani missenyi mkoa wa kagera, ndiko nilikozaliwa, ndiko nyumbani na ndiko nilikopewa urithi wangu wa shamba nk, ni nyumbani japo sikumwoa mke wajimbo hili

michuano ni mikali ya wagombea wa ubunge kupitia CCM na sijui itakuwaje

mpaka sasa kuna wagombea watano, wa kwanza ni yule aliyepo Deodarus Kamala ambaye wananchi wameisha mchoka ile mbaya, wa pili ni tajiri fulani aitwaye Balyagati, ana fedha nyingi huyu wa tatu ni Julius Lugemalila mfanyakazi wa mamlaka ya elimu tz wa nne ni Charles Katarama, afisa elimu wilaya ya biharamulo na ninadhani kuna tajiri mwingine aliyewahifanya kazi badarini dar na mwanasheria ndugu bernad mbakileki\

kinachonishangaza hawa jamaa sio wakazi wa jimbo hili wanalotaka kuliongoza wala sio wakazi wa wilaya ya missenyi, ni wenyeji wa Dar isipokuwa ndg katarama. wanakuja na pesa zao kununua kura, wanataka kusingizia kuongoza wananchi wasiokuwa wa kwao wasioishi nao wala nini

ni changamoto na nimshike mshike na sijui itakuwa vp maana kampeni za chini chini zishaanza na kumbuka sis ni watu wa fedha na sijui kama asiyekuwa na fedha atashinda au la

je mimi nina msimamo gani kama ilivyowahi semwa siku za nyuma?? bado ni mapema kusema lolote juu ya hilo ila harakati zinaendelea

6 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

"Isije ikafika wakati ili kupata wagombea wa udiwani na ubunge ikawa lazima kwa CCM kutangaza zabuni na anaye-bid zaidi au anayetoa dau kubwa, anachaguliwa kuwa mgombea."

Phillip Mangula, Katibu wa zamani wa CCM (http://216.69.164.44/ipp/nipashe/2007/09/12/98230.html)

Kamala, wakati wako ukifika sema tu wanablogu tutachangishana kama tulivyofanya kwa kijana wetu Nestory. Usikate tamaa.

NB: Dr. Diodorus Kamala nilikuwa naye jeshini Makutupora mwaka 1991 Operesheni Miaka 30 ya Uhuru Kombania B kwa afande Mwiba. Tayari alikuwa na chembechembe za "ukereketwa", uchapakazi na uadilifu. Tulikuwa tunamwita Mzee wa Sera aka Mzee wa Misimamo. Kumetokea nini mpaka wananchi wakamchoka???

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Kunichangiaaa?? karibu
kilichotokea labda ni mapozi ya kikwetu (kihaya) kupitiliza, kuzidi na kuwa mengi, amefikia hatua ya kuwatukana wapiga kura wake nk

chib said...

Huyo ameshalewa madaraka. Mambo ya kujisahau.

Mzee wa Changamoto said...

Na bado watakuja wengine wa upinzani hawajaja kuanza kudanganya wananchi.
Ndio zama za MAENDELEO ambapo tuna "tele-parliament.
Hahahahaaaaaaaaa

Mija Shija Sayi said...

Kamala usichelewe bwana, ingia na wewe kabla ya siku hazijasogea.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@damija, duh, kaziipo, nashindwa nianze vp, ngoja tuone ila yahitaji moyo