Saturday, May 1, 2010

blugo nishule kubwa

namnukuu mzee wa changamoto juu ya ushule wa blogu zetu, nimejifunza mengi katika kublogu hivi karibuni. ni matondo aliynifundisha juu ya umuhimu wa kusaidia wengine

nikiwa naishi katika jamii, nitatenga vimsaada vyangu vidogo vidogo kama viile kuwasaida wanafunzi wa shule za kata nk, lakini pia nitakuwa nikisheherekea sikukuu kubwa kubwa za kidini na nyinginezo kwa kutembelea ma hosptali na kuwapa pole wagonjwa, nitabeba sabuni, vyakula na vijisenti vichache kwa ajili hiyo

ni kweli kuna wengi wanasubila upendo wetu ili nao wajifunze kupenda, wengine wanasubilia sisi ili waweze kuwa na matumaini tena maishani . labda hata mimi nilimsubila Matondo ili nianze kuwasaidia wenzagu. ila hili litafanyika kimya kimya nikiogopa 'ego' isije ingnilia kati

hii ni shule niliyoipata kutoka kwa ndugu matondo katika ulimwengu wa blogu na ni shule kuuubwa kupitia blogu

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli Kamala blog ni shule. Kwa kweli tunajifunza mengi sana kupitia hizi blogg na kuna wakati hata wenyewe hatujui hili.

Fadhy Mtanga said...

Kaka Kamala nakubaliana nawe kabisa. Nami nimekuwa nikifikiria kuandika post juu ya faida za kublog.

Pamoja sana kaka.

Wikendi njema.

chib said...

Msisahau kublog nako kunatafuna sana muda na pesa pia kwa kulipia mtandao, pia nayo ni shule ya kubajeti!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@fadhy, andika tu na hizi ni mojawapo.

@chib ni kweli ni gharama lakini faida ni kubwa pia

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kamala - nilipoanza tu kublogu "ulinijia juu" kwa maoni yako ya kiutambuzi mpaka nikaanza kujiuliza kama kazi ya kublogu nitaiweza. Wakati ule nilikuwa nachemka sana mtu akinirushia madongo au kutoa maoni hasi kunipinga.

Napenda kusema kwamba wewe ulihusika sana katika kunifungua macho na kuanza kuyatazama maoni ya wengine kwa jicho pana zaidi, kuanza kuyaangalia mambo yote katika uwili wake na siyo kujibana katika mtazamo mmoja tu finyu. Ndiyo maana nikafikia kuandika posti hii: http://matondo.blogspot.com/2010/04/fikra-ya-ijumaa-wanablogu-tusiwe-na.html

Sikujua kama kisa changu cha Muhimbili kingekugusa na kukubadilisha: http://matondo.blogspot.com/2010/02/siku-niliyokutana-na-ubinadamu-wa-kweli.html

Mimi kama mwalimu huwa naamini kwamba katika kufundisha pengine mwalimu ndiye anayefaidika zaidi kuliko mwanafunzi na mwalimu asiyependa kujifunza kufundishwa na wanafunzi wake hafai. Tunablogu tukidhani kwamba tunawaelimisha, kuwaburudisha na kuwahabarisha wengine kumbe katika kufanya hivyo sisi wenyewe ndiyo tunafaidi zaidi kuliko hata hao tunaojaribu kuwafikia. Tuko pamoja!

Mfalme Mrope said...

nilikutana na dada mmoja akanieleza eti yeye haingii kwenye blog za kiswahili kwasababu hana cha kujifunza huku. Yeye ati huenda kwenye blogs za kiingereza. Binafsi mimi niliona huyu ana kasumba ya kitumwa kwamba kila kitu kilichoandikwa kwa kiinglishi basi ndicho chenye maana. Hajui kuwa material yaweza kuwa yale yale ila lugha tu ndiyo tofauti...

Fadhy Mtanga said...

Mfalme Mrope mimi nina marafiki zangu hawataki kabisa kusoma mashairi ya Kiswahili. Daima wananiambia kama nataka wawe wasomaji wangu, niandike ya Kiingereza. Kuna wakati nilianza kuandika, nikaona ni utumwa.
Sasa nipo katika kukamilisha mswada wa riwaya yangu ya Kiswahili. Huwezi amini rafiki yangu mmoja nilimwomba aisome na kunipa ushauri kabla sijatafuta mchapaji. Huwezi amini amesema hana interest na hadithi za kiswahili.
hivi ndivyo tulivyo waswahili. Mwalimu Nyerere alisema haamini kama wakoloni walifanikiwa kiasi hiki kutulisha kasumba.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yaaani usomi wetu bwana!