Monday, May 3, 2010

hivi sisi tunamiliki nini dunia hii?

binadamu yuko bizee katika kuhakikisha anamiliki vitu hata asivyohitaji, anashindwa kujua kuwa sisi hatumiliki chochote japo vitu vyote vipo ili sisi tuvitumie tu na kuviacha hapa hapa

eti unamiliki nyumba?? serikali ikiamua si inaweza kukunyanganya wakati wowote? eti unamili gari? si unaweza kunyanganywa au kuamrishwa usiliendeshee popote pale? eti unamiliki nguo, ni kweli?

mbona sasa vyote huviacha wakati wa kuviacha ukifika?? ehe?

eti labda unaumiliki mwili? mbona wa uacha (kufa)?? hata amani, upendo namafanikio, hatuvimiliki bali vipo kwa ajili yetu kuvitumia kwa wakati mfupi tu na kupenya.

hata nguvu sio zetu (hata nguvu kuu / MUNGU) bali zipo tuzitumie na kuziacha. kiuhalisia sisi hatumiliki chochote na wala hatumilikiwi na chochote pia au?? labda vitu vyote vipo ili sisi tuvitumie tu kwa muda na kuviacha

au sio??

1 comment:

Fadhy Mtanga said...

...hata wanaomiliki madaraka wanasahau watayaacha.