Wednesday, May 12, 2010

Jina la mtoto!

naomba ushauri wa juu ya jina la mtoto bila kujali jinsia. ila ni vyema likawa la kiswahili au kihaya. lisiwe la kunukuu vitabuni kama bible au korani. kama ni la kabila lako liwe na maana nzuri au positive
sitaki majina ya visasi kwa mfano mimi niliitwa Lutatinisibwa kama ujumbe wa baba kwa babu kuwa yeye haogofywi, sitaki hilo
naomba ushauri juu ya jina la mtoto wa mtu kama mimi jamani

14 comments:

Yasinta Ngonyani said...

akiwa wa kiume mwiteni Hyasint na akiwa wa kike Yasinta:-)

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mambo tayari eeh?

Akiwa wa kiume mwiteni Masalakulangwa - the intelligent one, au Jidulamabambasi - asiyeshindika!!!

Kama ni wa kike basi aitwe Koku(shubirwa) au Yasinta - ingawa sina uhakika na maana ya hili la mwisho!

Kuna kitabu kikubwa cha majina ya Kiswahili kilichoandikwa na Profesa Sharifa Zawawi. Nadhani kipo mtandaoni pia. Pengine itabidi ukitafute pia.

Mija Shija Sayi said...

Mwite Tanzania au Afrika.

Bennet said...

Akiwa wa kike mwite mamboza yaani mstaarabu na asiye na papara/mvumilivu

Anonymous said...

Mwite Moja (Emoi) bila kujali jinsia!

Ukijaliwa wa pili, mwite, Mbili (Ibili), na kadhalika!

Masangu, tulitumia kitabu cha Kiswahili mashuleni (shule za msingi) enzi za zamani. katika kitabu hicho, kulikuwa na "character" yenye jina, Masalakulangwa Mtoto wa Nyoka!

BAP

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Born Again Pagan (BAP);

Masalakulangwa Mtoto wa Nyoka! Duh!
Basi Kamala achana na hilo jina.

Katika hadithi nyingi za Kisukuma za kule Unyantuzu (Bariadi), Masalakulangwa ni kijana shujaa mwenye akili sana (masala) ambaye mara nyingi ndiye mwokozi na mkombozi wa jamii.

Huu ni utani na Kamala anatubabaisha tu hapa. Pengine tayari ana jina. Si ajabu mtoto akiwa ni wa kiume akaitwa Munga - kwa heshima ya baba wa taaluma ya Utambuzi nchini Tanzania Munga Tehenan.

mumyhery said...

Akiwa wakiume mwite Heri, akiwa wa kike mwite Furaha

SIMON KITURURU said...

Muite ``KICHWA ``

Au tu Kamala.

chib said...

Muite Mwerevu bila kujali jinsia
Baraka kama ni wa kiume
Malaika au Karungi kama ni wa kike

Anonymous said...

akiwa wa kike mwite bi.kidude,maana yake siijui

Egidio Ndabagoye said...

Ben Mkapa Junior

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe nabagoye wewe??? nini maana ya jina hhilo??

Subi said...

Nami napendekeza bila kujali jinsia:
- Subira
- Tumaini
- Furaha
- Bahati

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@Subi

jina la Subira silikubali sana, tumaini, bahati furaha wapo katika kaukoo tayari