Thursday, May 27, 2010

kuhusu uongo, wanaume wake na Yesu

katika mada ju ya uongo simon aliuliza;

uongo waSwali kwa Wakristo:

Hivi inawezekana Yesu aliwahi kudanganya eeh wakati anadunda hapa Duniani katika mwili wa Kibinadamu?


saasa binti wastara akasema kuwa wanaume hudanganya kuliko wanawake, sijui anajuaje hili jambo wakati yeye ni mwanamke, anajuaje wanaume walivyokuwa waongo bila wanawake??

ila wanaume hudanganya uongo mdogo mdogo na wanawake mkubwa, kwa mfano; mwanaume atakwambia nilikuwa mpirani kumbe alikuwa na nyumba ndogo, au ili mwanamke (hasa wasichana) akupatie unachotaka ni muhimu umdanganye unampenda, utamwoa nk. lakini kunatofauti gani kati ya ndoa na tendo la ndoa?? si huzalisha tu au yote ufanya watu wakae uchi sehem??

ila sasa uongo wa wanawake, utaona ni mrefu, kumbe kiatu ndo kirefu, utaona mweupe, kumbe krim, ataona ana hips, kumbe mavazi, utazipenda nywele zake, kumbe wigi nk nk


Sasa jamani eti nani mwongo kati ya mwanamume na mwanamama??????

3 comments:

Maisara Wastara said...

hivi bado huamini tu kuwa wanaume ni waongo kuliko....

Nipe muda nitakuwekea mada pale kwangu...
naamini utaujua ukweli

Mija Shija Sayi said...

Kwa maelezo haya, wote ni waongo.

Yasinta Ngonyani said...

Hakuna mtu mwongo kila mtu amewahi kusema uongo tena ule mkubwa na mdogo..LOL