Monday, May 24, 2010

lini tutakuwa chanya (positive)?


nimekuwa katika safari nyingi na yawezekana nusu ya maisha yangu sasa ni kwenye vyombo vya usafiri. ila nipendacho nikiwa kanda ya ziwa na historia ya bara bara mbovu, usafiri wa kiswahili na maji ya ziwa victoria

ukitoba bukoba mpaka musoma, kushoto kwako unaona ziwa victoria mpaka mwisho wa safari yako na ukirudi pia kulia kwako ni ziwa hilo na urembo wake. ila sasa ukitaka kuruka kwa ndege ni lazima upite juu ya ziwa hilo na kama ni mwa meli basi ni ndani ya ziwa hilo huku ukioga au hata kutawadhia maji ya ziwa hilo

ila sasa, binadamu inabidi tujifunze kufikiri vizuri, kuongea vizuri na kutenda vizuri. watu woote wanalalamika, basi likiwahi wanalalamika, likichelewa wanalalamika, likisamama ili wachimbe sumu wanalalamika kuwa limesimama pawazi au likisimama vichakani wanaogopa usalama wao. na hata ndege au meli hivyo hivyo

hivi ni lini sis tutajifunza kupokea kila jambo kama linavyokuja, tukalikubali na kujifunza na kunagilia mengineyo??

lazima tuwe chanya jamani
na tukumbuke kila jambo lina upande mwingine ambao lazima uwe mzuri tu

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

ntafurahi hiyo siku ambayo tutaweza kubadilika. maana watu hata wakila wanalalamika wameshiba na wakiwa na njaa wanasema wana njaa DUH! kazi kwelikweli. Ila nina imani tutafika tu.

Mfalme Mrope said...

Teh teh teh... Hiyo ni kweli kabisa. Tena haka ka wimbo kasemao eeh jamani, binadamu hatosheki, hata ukimpa nini, milele hatoridhikaa eeeh!!! Sidhani kama twaweza kuwa chanya milele kwani kutoridhika ni asli yetu.

chib said...

Kumbe Kamala wakati mwingine una fikira murua :-)
Usikonde, natania, ila nimependa somo la leo!