Friday, May 7, 2010

Mawazo ya Kutongoza na kutongozwa = wewe
Simon Kitururu aliwahisema maajabu ya kutongozwa ni kwamba mtongozaji hawezi mwambia mtongozaji kile anachokitaka kwani ataonekana chizi, jinga, dhalilishaji nk. Mtu atamsifia mwingine nywere zake, guu au hata kifua kama sio ndevu ilihali akijua akitacho sio hicho akisifiacho!

Lakini pia mtu atakukaribisha nyumbani eti uje upaone au tupige story au mwende gesti ili mpate uhuru wa kuongea na kuchati badala ya kukwambia lile atakalo. Akisema atakalo ni vigumu kulipata lakini akisema asilolitaka hapo kashinda mchezo

Sasa koero kalalamika anavyotongozwa na sijui kwa kweli ni kwanini analalamika laivu inawezekana kuna vitu avipendavyo. Kama wewe umewahi tongoza, basi tukubaliane kuwa wakati huo ni wakati wa ufundi mkuubwa na baada ya kutongoza unaweza shangaa ni kwa jinsi gain maneno mazuri yalikutoka bila kujiandaa wala nini

Ila sasa matokeo ya kutongozana huwa ni makubwa kuliko watongozanao walivyodhania. Wakifanya jambo ambalo jamii hujifanya kutokuklifahamu nakulichukia wengine hulikemea vibaya sana na kulipachika matusi, matokeo huwa ni wewe au mimi au yule na wale

Asilimia kuubwa yaa watu uwaonao basi wametokana na suala hilo. Jaribu kujiuliza wakati wazazi wako wanafikiria kufanya tendo liliokufanya wewe uzaliwe, walikuwa wanafikiria nini? Ujinga upuuzi na uwongo kibao. Wazazi wangekuwa watoa siri, ungejishangaa ulivyozaliwa kwa njia za maneno ya kijinga kipuuzi nakipumbavu achana na tendo lenyewe

Ndio maana wakristo hudai kuwa Yethu hakutundikwa mimba na mtongozaji yeyote maana ni aibu mfalme kuzaliwa kwa “ujinga” huu

1 comment:

Fadhy Mtanga said...

Ha ha haaaaaa
Sanaa ya kutongoza ina kaubunifu sana. Maana una strago kuhakikisha mtongozwaji anaingia kumi na nane zako