Thursday, May 20, 2010

mhindi na mahindi


nilipokuwa nasoma chuo cha ushirika mjini moshi nilienda kununua Hindi la kuchoma, kabla sijanunu akatokea mwanafunzi mwenzetu mwenye asili ya Asia yaani Mhindi (Indian) akatoa pesa na kusema naomba mhindi.


nilishangaa kuona mhindi ananunua Hindi. nikasema basi mimi nipewe mchina! yule Mhindi (mtu siye chakula) alinichukia na kutamani kunimaliza haraka sana.


ila ni changamoto, yale yale ya wahaya na haya, Wachaga na Chagga (za kitanda, eti mchaga anasema kitanda chake hakina chagga), Uchina na Uchi-na, nknnk

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ngonyani na nyani
kujua na jua
maua na ua
moshi mji na moshi kama moshi..lol

John Mwaipopo said...

twende kizungu kidogo.

bata mzinga anaitwa turkey, pia kuna nchi inaitwa turkey. turkeys huliwa sana siku ya sikukuu inaitwa thanksgiving. turkeys wangalijua mass destruction ya thanksgiving wasingalikuwa wakizaliana