Monday, May 3, 2010

nafasi ya Yuda katika kufanikisha kazi ya Yesu Kristo

Yuda Iskariote katika biblia analaaniwa na kila mkristo wa leo kwa kumuuza na kusuka njama mpaka kumsulubisha Yesu Kristo.

siku ya moja nikiwa naangalia ibada ya wakatoliki katika luninga moja, nilisikia wakitajwa 'watakatifu', akatajwa bikra maria, Yoseph, petro nk, kijana mmoja niliyekuwa naye akauliza, na Yuda je?

nami nikazinduka na kushangaa ni kwa nini Yuda asiheshimiwe kwani alikamilisha mpango. Kama Yuda asingekuwa Jasiri wa kumuuza Yesu, basi ile kazi ya Yesu aliyokuja kuifanya, Yaani kufia watu msalabani isingefanikiwa hata kidogo

sasa je kwanini tusimmheshimu nakumpenda Yuda aliyekamilisha mpango huo uliomleta Yesu kristo? kwa nini Wakatoliki wasimwite Yuda mtakatifu pia??

najiuliza tu wandugu

2 comments:

Fadhy Mtanga said...

Leo kijana umenifikirisha sana na kujiona mpuuzi kwa kuwa namwona Yuda kimeo siku zote. Yuda kumbe anastahili heshima tena kubwa na ya kipekee maana alikuwa na ujasiri wa kutengeneza mazingira ili mwana wa Adamu aikamilishe kazi yake.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

enhee! hapo patamu!

Zamani lakini si zamani sana nilikuwa na bifu na yuda kwa sababu tuliambiwa kuwa ni noma.


kwa kweli anastahili kuitwa mtakatifu kama si mtakavitu....lol