Wednesday, May 5, 2010

ni Munga Tehenan day

ni siku ambayo mwalimu wangu wa utambuzi, meditation nk aliondoka zake kwenye mwili. niliwahi andika mwakajana juu ya hili soma hapa sasa ni mwaka mwingineo umepita

Munga alikuwa akituaga lakini tusielewe anakwenda wapi. Munga alikufa akijua kabisa kuwa atakufa, ni kifo chema na kizuuri sana alichokutana nacho na ambacho nakitamani sana pia.

ni vyema sis kama wajumbe wa FAJI (familia ya Jitambue) na wafuasi wa mafundisho ya huyu jamaa kuiteua siku hii na kuiita siku maalumu ya Munga au kwa kiingereza Munga Tehenan day.


napigiwa simu na watu wengi wanaotaka kupata maarifa haya ya utambuzi, na mpaka sijui nifanyeje, lakini natafutwa kwa sababu ya huyu jamaa Munga tehenan, kuamua kunigawia haya maarifa bila gharama yoyote, alitumia muda wake na nguvu zake wakati mwingine na gharama zake kutoa maarifa haya kwa wengine bure kabisa

natamani kuiganyayo zake na namshukuru sana kwa ili, kwa kweli alibadilisha maisha yangu yoote.

7 comments:

chib said...

Gawa bure tu nawe, hakuna cha ... au....

Yasinta Ngonyani said...

Jamani kumbe ni leo miaka miwili tangu atutoke ingawa sikumfahamu lakini nimezisoma kazi zake nyingi sana kuanzia vitabu hadi magazeti na pia nimekuwa nimezipenda sana kazi zake na pia kuzitumia nadhani wengi mnajua nimekuwa natoa kazi zake hapo kwangu. Ni jambo la kusikitisha sana kumpoteza mtu kama wewe umetuacha lakini kazi zako nna sifa zako hazitakufa tutazienzi milele kwani ni kazi na maarifa mazuri sana.
Pia napenda kuchaukua nafasi hii kuwapa pole dhangu za dhati wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki pia wanafunzi wote.a labda Tanzania kwa kumpoteza mtu muhimu baba, kaka, mume, mwalimu Munga Tehenen. Ustarehe kwa amani popeni amina. UPENDO DAIMA-

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@CHIb, ulidhani natoza pesa?? njoo ujionee

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

RIP Munga

Mzee wa Changamoto said...

Kuna sehemu ya mafuzo yake ambayo tayari unaigawa tena kwa uwanja mkubwa kuliko aliokuwa nao. Unaeleza misimamo na kuitetea kwa kuwa unaamini unachoamini kutokana na alichokufunza Munga.
Unaandika na kueleza kile kilicho "zao" la mafunzo ya Munga na watu wanasoma (japo wapo wasiotoa maoni ama kusema kuwa yanawafaa).
Uzuri wa elimu ya kujitambua ni ubaya wake. Kuwa mtu anaweza kutotambua kuwa kajitambua mpaka ahitaji suluhisho linahitaji utambuzi. Wapo waliotambua umuhimu wa kukubali kifo cha mpendwa wao lakini hawawezi kulitambua hilo mpaka mpendwa wao afe. Ina maana hapo ndipo watakapoweza kutumia vema mafunzo tuyasomayo kwenu.
Binafsi sikuwahi kumjua Munga na najua sitaweza onana naye ana kwa ana. Lakini HAZINA aliyoiacha ndiyo inayonifanya kuandika ninayoandika. Ni kwa kuwa nilimsoma katika Jitambua na kuanza kuyaangalia mambo katika mtazamo mwingine, na kwa kuwa naendelea kukusoma, kumsoma Kaka Kaluse, makala zake kwa Da Yasinta na Da Koero na hata TAFAKURI ambazo zatokana na mafunzo yake kwa watu mbalimbali, nami najifunza, kisha nafunza.
Ufunzayo ni mengi na hakuna haja ya kutothamini kazi uifanyayo. Fanya lililo ndani ya uwezo wako kwa sasa na muda ukiruhusu, utaongeza juhudi.
Lakini umekuwa kama waya uunganishayo chaji (Munga) na taa (sisi)
Ni Munga Tehenan Day na sote twakumbuka aliyotufunza.
Tumshukuru yeye na walioenda kinyume na utambuzi kumfanya ajikite "kuweka mambo sawa"
Blessings

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Riwaya yake ya Rais wa Kesho inabidi isomwe na kila mtu....

Anonymous said...

Asante sana kwa kutukumbusha siku ya Munga. Nguvu aliyopanda itaendelea daima milele. Kama unavyofahamu pamoja na kazi zake nyingi aliacha Familia ya Jitambue FAJI. Umoja huo bado unaendelea na madarasa Kimara Rombo. Kwa wale wanaohitaji kujuinga tunaomba wape maelekezo. Siku za usoni FAJI kwa kushirikiana na mama Munga, inatarajia kuanza kuuza DVD za masomo ya Utambuzi za Munga. Pia kuchapisha vitini na vitabu. Kazi unafanya kueneza utambuzi ni kubwa tunakupongeza sana pia uwepo wako kimwili Dar tunauna. Karibu FAJI Mbeyella