Monday, May 17, 2010

sara yetu hii hapa-- utunzi wa mtktf Francis


Mungu, nifanye niwe nyenzo yako ya amani;

penye chuki, pandikiza upendo;

penye jeraha, samehe;

penye kukosa maelewano, unganisha;

penye wasiwasi, tia imani;

pale penye kukata tamaa, weka matumaini;

pale penye giza, tia mwanga;

pale penye huzuni, tia furaha.

Mungu, nipe kile ninachoomba kisiwe cha kunifariji ila

kiwe cha kuwafariji wengine.

niweze kueleweka na kuelewa,

niweze kupendwa na kupenda.

kwani tutoavyo ndivyo tupatavyo,

ni katika kusamehe ndipo nasi tunasamehewa,

na ni katika kufa ndipo tunazaliwa kwenye maisha ya milele..

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

amina! ni sala nzuri sana.