Friday, May 14, 2010

"Tunaoambiwa tupungue ni sisi masikini na hasa Waafrika kwani "wenye dunia" wana wasiwasi kwamba siku moja tutalemewa sana na dhiki na tutafanya "massive migration" kwenda kwenye nchi zao.Cha ajabu ni kwamba wenyewe ndiyo wanatumia karibu raslimali zote na wametawala kila kitu. Badala ya kujaribu kuleta usawa katika umilikaji na utumiaji wa raslimali za dunia, suluhisho lao ni kutulazimisha tuache kuzaana kwa visingizio kwamba eti dunia itafikia mahali itaelemewa. Ndiyo maana kuna watu wanaoamini kwamba magonjwa mengi ukiwemo UKIMWI ni mojawapo ya mbinu za kutupunguza sisi masikini. ".....
asema Matondo

2 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mara nyingi maoni yanapotolewa katika muktadha wake yanakosa ladha iliyokusudiwa. Ni vizuri mara zote kuutambulisha muktadha ambamo maoni hayo yalitolewa.....

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

asante kwa ushauri, nilipitiwa