Wednesday, May 26, 2010

Uongo na Ukweli vyoote vina kiini kimoja

kuna hadithi nyingi sana juu ya uongo na ukweli na ukweli na uongo. wengi wanajifanya kuuchukia uongo japo ni waongo lakini wasichotaka kujua ni kuwa uongo na ukweli vyote ni kitu kimoja au vina kiini (essence) kimoja au kilekile
kumbuka bila uongo hamna ukweli na bila ukweli pia hamna uongo. hata katika biblia kuna mwanamama kwa jina Rehab aliyesema uongo ili kuokoa majesha ya Joshua yasije angamizwa na yawaangamize adui
sisi ni waongo na tunauishi uongo. kama tunataka ukweli ni lazima sisi wenyewe tuwe wakweli kwetu sisi wenyewe na wengine
ila sasa inategemea na matokeo ya ukweli wako au uongo wako mweyewe. je useme ukweli na watu waangamie ili ionekane umesema ukweli au useme uongo na kuokoa wengi?
matokeo ya ukisemacho ndiyo muhimu na sio ukweli au uongo. madaktari kama Chibuga huongopa sana, kwa mfano, mgonjwa kaja na presha iko juu, ni lazima umdanganye ili aweze kuipokea kama kawaidia, ila ukimtisha au kumwambia ukweli ulio uchi, ataogopa, itapanda zaidi na labda atakufa (japo kufa sio kubaya), ila ukimdanganya mambo yataenda muswano
hata katika ndoa zetu ni lazima tuuishi uongo pale ambapo ukweli unaweza hatarisha ndoa zetu (hili linaeleweka zaidi)
Ukweli na Uongo ni kitu kimoja, vinafanana na vina umuhimu ule ule

7 comments:

Markus Mpangala said...

kuna uwongo mzuri na uwongo mbaya? duh mkuu! nilikutana na hilo mtaa fulani nyeti nikakuta vigogo wakimwaga maneno ati kwa wananchi wanamwaga uwongo mzuri! heee! sasa kama uwongo ni jambo linaloendana na ukweli basi kuna mengi ya kujiuliza ukweli ni nini na uwongo ni nini?

wakati mwingine tunaposema tamathali za semi kwamba 'ametia chumvi' nadhani huo nao ni longolongo au? Jabali Kamala ubarikiwe na mungu wa wahaya

SIMON KITURURU said...

Swali kwa Wakristo:

Hivi inawezekana Yesu aliwahi kudanganya eeh wakati anadunda hapa Duniani katika mwili wa Kibinadamu?

SIMON KITURURU said...

Swali kwa Waislamu :

Kuna Mdau hapa ambaye anaweza kunitonya hii kitu iitwayo TAQIYYA


.... ambayo inasemekana inaruhusu Waislamu wa SHIA kuitumia katika kitu kitafsiriwacho na baadhi ya watu kuwa ni ``DANGANYA kama ukidanganya kunauendeleza UISLAMU´´?

Maisara Wastara said...

Kama kuna viumbe waongo hapa duniani, basi ni wanaume...
haki ya nani! ni waongo kweli..

katawa said...

Mtakatifu yawezekana yesu aliwadanganya watu hasa pale aliposema yeye ni njia ya kwenda kunako uzima bila yeye hakuna njia nyingine,je wewe unayaamini aliyoyasema?

katawa said...

Mtakatifu,yawezekana yesu alidanganya hasa pale aliposema yeye ni njia ya kwenda uzimani pasi yeye hakuna maisha ya milele.Je wewe unayaamini maneno yake?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@ katawa swali zuri, mimi natayakubalije wakati sikukambiwa mimi??i nayasoma tu kwenye vitabu??

naamini kitu live na sio past, kama anageyasema leo ningnekubali ila