Monday, May 10, 2010

... Wakipungua watu labda AMANI itaongeeka... asema damija.mwanamke wa kisu, panga, mkuki mpaka SHOKA a.k.a Damija (pichani) anadai ya kuwa watu wakipungua ndo amani itaongezeka, je ni kweli??

kama damija anaamini hivyo ni kwa nini ana Mume (kaolewa) ili asiwe peke yake-- wawe wengi na kikubwa zaidi kazaa, kwa nini kama anaamini wingi wa watu unaleta vurugu azae a.k.a kuongeza idadi ya watu??

binadamu kwa ujinga uliojificha katika madai ya busara anadai wingi wa watu unahatarisha maslahi au raslimali na kwa hiyo anahaha kuzuaia ambao hawajazaliwa wasizaliwe, lakini binadamu huyo huyo anahitaji kuwa na wenzake wengi ili aweza kupata na kutumia rasilimali hizo je tukipungua amani itakuwepo??

kwani binadamu ni wengi kuliganisha na nani haswa?? si kuna viumbe wengi kuliko binadamu mwenyewe?? mbona havipunguzi??

kama ishu ni raslimali, mbona sasa anaziacha ziendelee kuwepo yeye anapokufa, si aondoke nazo tu??

najiuliza tu

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kazi kwelikweeeeli hapa. Kamala kwani huna amani au haitoshi hii amani? "wakipunga watu labda amani itaongezeka" lakini mbona wanazidi kuongozeka

Fadhy Mtanga said...

...sijui nani aanze kupungua halafu sijui nani aache kuongeza watu

kARIM (Mbezi Beach) said...

Da Mija hapo ni yupi. Mbona wote wanafanana hawa. Lakini wazuri duh! Ningekuwa sijaoa nami ningemsaidia mmoja wao kuongeza idadi ya watu ingawa anapigana watu wapungue...LOL

Mija Shija Sayi said...

Wewe Kakangu kamala wewe! hata picha ulikoipata.

Haya, kama si hivyo nidhanivyo mimi unadhani ni kwa nini dunia inahangaika kupunguza watu? Inaogopa kwamba watu wakizidi na maarifa yanazidi, bora wapungue waondoke na maarifa yao.

NI DALILI YA KUTOJIAMINI.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

safi sana damija.
@Karim kweli binti kaumbika huyu

Bwaya said...

Suala la kupungua kwa watu juu ya uso wa dunia halihusiani na shauku zetu kama viumbe. Mduara uliojitengeneza kimaumbile unatulazimisha kupungua bila hiari. Kwa mfano, tunawajua viumbe wengi wa kale ambao walilazimishwa kuondoka bila hiari yao. Mazingira yalibadilika mno kiasi cha kutoweza kuwalinda tena.

Sasa kwa jinsi mduara wa kimaumbuile ulikofikia, ni wazi kuwa wanadamu kwa sasa watalazimishwa kuishia kwa lazima wapende wasipende. Na hili limeanza na tunaliona.

Njaa. Majanga ya asili. Migogoro. Magonjwa. Utasa na kadhalika.

Pamoja na kwamba inapendeza tuendelee kuwa wengi, lakini ni wazi kiu hiyo haitakidhiwa na maumbile.

Ingekuwa poa sana kama pangekuwa na namna ya kusuluhisha mlinganyo huu pasipo kulazimisha kupungua kwa idadi ya watu ambao hao hao wanapambana kuuana na kuharibu makazi yao kwa hiari ama shinikizo la idadi yao.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@ bwaya nakunukuuu....

Njaa. Majanga ya asili. Migogoro. Magonjwa. Utasa na kadhalika......


unadhani kuna wakati haya majanga hayakuwepo duniani?? unafikiri ni kweli binadamu wataisha siku moja?? kwa nadhalia ipi ya evolution au creation??

je unafikiri kuwa tuna mwisho kweli sisi au mwanzo?

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Tunaoambiwa tupungue ni sisi masikini na hasa Waafrika kwani "wenye dunia" wana wasiwasi kwamba siku moja tutalemewa sana na dhiki na tutafanya "massive migration" kwenda kwenye nchi zao.

Cha ajabu ni kwamba wenyewe ndiyo wanatumia karibu raslimali zote na wametawala kila kitu. Badala ya kujaribu kuleta usawa katika umilikaji na utumiaji wa raslimali za dunia, suluhisho lao ni kutulazimisha tuache kuzaana kwa visingizio kwamba eti dunia itafikia mahali itaelemewa. Ndiyo maana kuna watu wanaoamini kwamba magonjwa mengi ukiwemo UKIMWI ni mojawapo ya mbinu za kutupunguza sisi masikini.

Bwaya said...

Kamala nitakujibu swali lako mapema. Ila kwa kifupi si nadharia ni maumbile. Kamuda kameniishia hapa