Monday, June 21, 2010

Bukoba ni sherehe za injili

ni sherehe za injili ya KKKT kufika hapa. ni miaka mia tangu mwanzoni mwa 1900. alikuwepo kikwete na wadhungu lukuki. ni sikukuuubwa hapa

ila sasa. watuwanasheherekea injili huku injili ikiwa hoi kiasi chake, hoi bin taabanyale yaliyopaswa kuhubiriwa yako pembeni na mambo ya dunia yana nafasi kuubwa sana kuliko yaaaminikayo kuwa ya mbinguni. ni biashara namisheherekeo mingi tu.

karne ya injili ilibidi tuone mabadiliko chanya ya ujio wa watu wa Mungu na sio hasi yaani wachunga kondoo kufanya yale wayazuiiayo.

ni wakati kama huu tulipaswa kuona mengi na makubwa. ila ni vyema, tumeona mengi mimi nimekulia na kulelewa kwenye nyumba za KKKT na wazazi waajiliwa wa KKKT

injili ina faida lakinisio hii ya sasa, inaenda kombo

askofu wa dayosisi ya huku anaonekana kutokusoma alama za nyakati na kushikilia misimamo ya zamani kanisani na jinsi ya kuendesha ibada. anapenda ibada iendeshwe vile yeye alivyofundishwa au ilivyoendeshwa alipomkuwa mdog na sio vile kizazi cha sasa kipendavyo

ni karne ya injili na ni sherehe kuubwa hapa mkoani kagera.

sherehe hizi mpaka kijijini kwetu, nilishuhudia famila ya baba yangu ikisheherekea na kujumuika kumshukuru mungu na mama yao (bibi yangu) japo famila hii kama familia bado ina mengi ya kufanya, mengi ya kukpitia.

ni sherehe, ni karne ya injili, tunasheherrekea kwa nje yetu, sio ndani mwetu, sio kuanza na familia zetu ila ni jamii ituone tulivyo wakrsito na sio kuuishi huo ukristo wa kweli

3 comments:

chib said...

Tunatumaini na watu watatakasika sasa huko au wasemaje Mkuu!

Anonymous said...

Kweli hata mimi suala hilo lilinisikitisha kuona watu tunakimbizana au tunahangaika kusherehekea kimwili badala ya kiroho(inauma)
Wakristo wametangaziwa na kuhamasishwa kununua Tshirt za Jubilii na kitabu kinachoeleza Miaka 100 ya Dayosisi.Kuna maelfu ya Tshirt. Bila shaka ingekuwa ni furaha kubwa kama idadi ya Tshirt zilizouzwa ndo watu waliokata shauri ya kubadili maisha yako na kumrudia Mungu.
Kamala ubarikiwe

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

asanteanony kwa kulona nililoliona pia