Wednesday, June 16, 2010

eti Mungu ni nani??

katika moja wapo za mitundiko hapa kijiweni damija aliniuliza swali juu ya Mungu, eti Mungu ni nani au ninini au ni kitu gani.

tuna definitions kibao ila lijapo suala la Mungu watu huongelea uumbaji na umilikaji wa kila kitu tukijuacho na tusicho kijua na baada ya hapo wengine huleta vitisho kwamba anaweza kutuuwa sote na ipo siku atatuchoma moto.

wapo waongeleao upendo kama vitabu vya dini lakini upendo wenyewe wakati mwingine ni wa kutilia shaka na wasi wasi kibao. ila sasa ukisoma vitabu vya dini, bila shaka unahitaji msaada wa kuvitafsiri juu ya Mungu. lakini akutafsriaye akiwa na lengo la kuendelea kukuchuna pesa kwa mfumo wa sadaka atakutishia mpaka umpe pesa kidogo.

ukisoma biblia na hasa agano la kale unaweza kushangaa juu ya alivyo na afanyavyo kazi Mungu wa wakristo a.k.a Mungu wa Israel. anallipiza visasi, anaua, anaadhibu na kutwanga watu viboko kibao. unaweza kumuongopa mungu huyu japo yesu alisema ni wa upendo

lakini Yesu alisema Yeye pekee ndiye njia ya kwenda kwa Mungu. anyway, binadamu tunajiona kama tunamilikiwa na Mungu badala ya kujia kwamba sisi na yeye ni kitu kimoja.

ni somo gumu, ila tumtafute ndani mwetu then tutaanza kumuona katika kila kiumbe na katika kila kitu

3 comments: