Saturday, June 12, 2010

kombe la dunia, ni wakati wa mihemko


nikiri kwamba mimi sio mpezi wa michezo mingi duniani na ni kiri kuwa mimi sio mshabiki mkubwa wa soka, ila ukweli ni kwamba huu ni msimu wa kombe la dunia linaunguruma. ni kati ya michezo niiangaliayo sana. huwa sipendi kuangalizia mpira kwa jirani au baa kwani mimi napenda uhuru


huwa nakimbia nyumbani kuangalia mpira kwa utulivu bila kuwa na machknow au washika limoti na kubofya bofya wala kuwa na watazamaji wanaoshangila mpaka presha ikapanda


nikiangalia mech za ufunguzi, nilijikuta nikishangilia vibaya na shemeji yangu baada ya bafana*2 kkufunga bao lao. yaani ni mhemko kwa kwenda mbele ile mbaya.


ila sasa ngoma nzito, nilisikia watu wakishangilia hata nje kwani mimi nakaa kwenye kotaz fulani. najiuliza ikitokea tanesco wakakata umeme iatakuwaje au TV ilete chenga, wewe


kuna washangiliaji mpaka wakajinyea na matatizo mengine


ni wakati mwinngine wa mihemko, kuhemkwa kushangilia na kusikitika.


ni kombe la dunia bondeni

No comments: