Thursday, June 24, 2010

kuingilia

hivi ulishawahi kujiuliza juu ya suala hili la kuingilia?? na labda tujiulize kuingilia ninini?? kuna waingiliao ndoa, kazi, maisha, mazungumzo, safari, tamaduni na kuingilia kwingi mno

kuingilia hasa pale kabala ya wakati wetu huleta matatizo mengi sana na watu hawajifunzi. mtu anaongelea jambo, jamaa anaingilia na kusema ya kwake na hishia kubadilisha maana nzima ya hadithi au kusema yale ambayo yangesemwa tu mwishoni

unakuta watu wanapigana, sauti ya ndani mwako inakushauri kuachana nao, unaingilia ugomvi ule na kuchomwa kisu au kuumizwa au kupelekwa kuwa shahidi wa yaliyotokea

kuingilia ni soo jamani. Wanandoa au wanandugu wanagombana, unaingilia harafu baadaye wanapatana unabakia kuonekana kama mleta matatizo badala uwaache wayamalize wao wenyewe kwa wakati wao na kwa mitizamo yao. hizi ni hatari za kukingilia.


kwa nini tunaingilia??ni kwa sababu hatuko katika utulivu na sisi wenyewe au hatuna urazini, hatujiulizi tunaona kila mahala panafaa tu kuingilia na kuonyesha ujuaji wetu au umwamba wetu au kujali kwetu au uwezo wetu au ukuu wetu na tunaishia kuharibiana mambo yetu. ni kwa kuingilia

kama tukimeditatate na kuwa katika utulivu na sisi (self conscious) tutakuwa wasikilizaji na watazamaji kwa sana ha hivyo kujua nafasi zetu na kuacha wengine wawe wengine nao wacheze nafasi zao pia

jamani tujihadhali dhidi ya kuingilia pale tusipopaswa kufanya hivyo ila tuwe sisi na kucheza nafasi zetu kamili.

2 comments:

chib said...

Kuna watu huwa wako kimbelembele kwenye kila kitu, hivyo huona kila mahali wanapaswa kuonekana wametia neno.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chib to mfano kati ya bloggers wenzio!!!