Saturday, June 26, 2010

najiuliza ingekuwaje ingechezwa mipira miwili?/


hivi ingekuwaje kama uwanja mmoja ingechezwa mipira miwili tofauti badala ya mmoja kama tulivyozoea?? ehe! ingekuwaje na wachezaji wangechechagua wacheze mpira gani?? si wangekuwa na uhuru wa kuchagua mpira wa kuchabanga badala ya kubanwa kucheza huu mmoja??

je ingekuwaj kama sheria ya mpira ingeruhusu gorikipa wa timu pinzani kudakia timu nyinginne??kwa mfano, mechi kati ya ghana na ujermani, kipa wa ghana alinde gori la ujermani na wa ujermani alinde la ghana?? ingekuwaje lakini???
najiuliza, ingekuwaje kama wachezaji wote wangekuwa wanagombania kufunga gori?? yaani kila mmoja anataka kufunga yeye??

lakini ingekuwaje kama refa angaruhusiwa kuingia na kiboko uwanjani na kuwatwanga mijeredi wachezaji badala ya kadi??/

lakini ingekuwaje kama padri, shehe au askofu angekuwa uwanjani kwa lengo la kuwalaani ili waende motoni wale wachezaji wanaokiuka maadili??
je ingekuwaje, ingekuwaje na itakuwaje kama ikiwa????

najiuliza tu bajameni,

2 comments:

Candy1 said...

duuuh Kamala...bado nusu nianguke baada ya swali la tano

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

angukatu cangdu au unasubili msaada wa kuangushwa??