Monday, June 14, 2010

ni jubilei miaka mia moja KKKT - DKMJ

mji wa Bukoba sasa uko katika vifijo na ndelemo, kuanzia jumatatu hii ni wakati wa vifijo na nderemo kwa wafuasi au waumini wa dini ya kilutheri ya kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania dayosisi ya kasikazini magharibi (KKKT-DKMG)

ni miaka mia tangu ulutheri ufike maeneo ya Buhaya/kiziba/bukoba na hata karagwe ukitoke nchini uganda. taarifa zinasema kuwa JK atakuwepo katika shamla shamla hizi. mojawapo ni mahubiri ya nguvu na kuweka jiwe la msingi katika chuo kikuu kinachotarajiwa kuanzishwa hapa Bukoba al maarufu kama JOKUCO

nyumba zimepakwa rangi nk. ila swali la kujiuliza ni kama je itakuwaje baada ya miaka mia mingine kupita?? KKKT itakuwepo?? kanisi lisilowekeza kwa vijana litakuwepo kesho kweli??

na je ni matunda gani tumezaa kama kanisa au wakristo?? je wanafunzi wanaosoma na kuhitimu kwenye vyuo mbali mbali vya kanisa / dini wanaonyesha maadili gani ya kikristo au tofauti wawapo kazini na kuwa ni mfano wa kuigwa?? kwamba sio mafisadi, wanatenda kazi kwa bidii?? je wanaishi je huko kwao kwamba ni wasafi wa kuigwa au nuru ya ulimwengu kama biblia inavyowaasa???

ni miaka mia ya jubilei na familia yangu inamunzi bibi yetu pia

2 comments:

Anonymous said...

Kamala, Jubilee ni Miaka 50 na Centennial ni Miaka 100!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@Anony wao wanaiita jubilei!!!