Tuesday, June 8, 2010

pesa na utaifa kwenye mpira wata TZ vs Brazil

nikubali kwamba mimi sio mpenzi saana wa michezo na sio mpenzi wa mpira wa miguu pia. ukweli napenda Volleyball na ndiyo mchezo wangu na kila siku huwa nafanya zoezi kila siku ya Mungu. ila sasa afya yangu sio njema sana. naumwa na hivyo nawahi nyumbani kupumzika. jana nikajikuta katika mapumziko yangu nikishuhudia mechi ya tafa nyota na Brazil
katika mechi hiyo, kuna watz waliokuwa wakiishabikia Brazil na m-brazil aliyekuwa akiishangilia nyotaz, ni kocha Mximo, aliishabikia taifa stars na kuuukana uzalendo wa Brazil. hivi unafikiri kama taifa Stars ingeshinda, maximo asingenyanganywa uraia wa nchi yake???, lakini unadhani Maximo aliishangilia stars kwa moyo au aliimarisha kibarua chake ili nyumbani waone anavyofanya kazi kuubwa na sio kule pesa tu..
hara imajini taifa stars inacheza kombe la dunia, inafika fainali na kukutana na Brazil kwa kocha m-Brazil a.k.a Maximo na inashinda na kuchukua kombe la dunia, unadhani Maximo atakaribishwa tena nchini kwake kwa ushujaa baada ya kufundisha timu pinzani na kuishinda timu ya taifa lake?? wakati akishangilia, unadhani maximo anaishangilia stars kwa moyo au anashangilia kibarua chake kwa nje huku ndani anaishangilia brazli??
najiuliza mimi jamani huku nikiendelea kupona kwa kasi

4 comments:

Markus Mpangala said...

nimekumbuka hoja za kocha wa Arsenal, Profesa Arsene Wenger. kwamba HIVI WEWE NI KOCHA WA TIMU YA TAIFA LA KIGENI HALAFU UNAPAMBANA NA TAIFA LAKO KATIKA MECHI, UTAIMBA WIMBO GANI WA TAIFA? JE UTAIMBA WIMBO WA TAIFA UNALOFUNDISHA AU TAIFA LAKO LA KUZALIWA??

Mkuu NIMETIKISA KICHWA HAKIKA SITANII hoja makini hii

chib said...

Siku hizi watu wanaweka maslahi mbele, kwa hiyo hawaangalii utaifa bali kibarua chao na misifa.

SIMON KITURURU said...

Yoyote atakaye jibu maswali ya Komandoo Kamala labda KUNAUWEZEKANO anadanganya kwa kuwa KARIBU MASWALI YOTE nahisi mwenye jibu sahihi INAWEZEKANA ni Mbrazili aitwaye MAXIMO.:-(

Nakuna kichwa lakini kuhusu topiki hii!:-(

Anonymous said...

Na tukiendeleza hoja hii kugusa uraia wa nchi mbili..utabaini kuwa una taabu zake, kama hizo!