Tuesday, June 1, 2010

shukrani kwako

najisikia deni la kukushukuru hasa wewe unayenitembelea mahali hapa na kunisoma kila upatapo nafasi. nakushuru zaidi wewe uachaye maoni kwani maoni yako hunifunza, hunisahihisha na unitia moyo pia.
kuna watu wanaonipigia simu na wengine kunitumia email katika kuelezea furaha zao juu ya kijiwe hiki. wengine hunitumia hata mada za kutundika hapa


hivi karibuni nimepokea simu ya mdau wa arusha akinidondoshea misifa na kujisema kuwa yeye ni mfuasi makini wa blogu hii
kwa kweli naniaendela kuwa kwenye uwanja huu wa blogu kwa sababu yako wewe unayenisoma, nazidi kuelika na kupata marafiki kwa sababu yako wewe unayetundika maoni na burudani kweli kweli

urafiki unaongezeka na sasa nina ndugu kila kona, ni kwa sababu yako kuendelea kunisoma. mwanifanya kujisikia mwenye deni pale shughuli zinibanapo na kushindwa kuweka mada mpya na kwahi ni kwa sababu ya kunitembelea kwenu nami nakuwa na moyo na najisikia kuendelea kublogu

Asanteni sana bajameni

4 comments:

Nuru Shabani said...

Kama binadamu hatuna budi kushukuru kwa kila jambo ambalo linatutokea katika maisha yetu, kwani kila jambo kuna kitu cha kujifunza, na unapojifunza ndipo unaelimika.Tunawaombea kila lililo jema mnaoblog wote na wachangiaji wote tuzidi kuelimishana.

chib said...

Mimi nakushauri upunguze utani!! Hasa pale unapotembelea blogu myingine :-)

Yasinta Ngonyani said...

Usengwili!

Mija Shija Sayi said...

Asante pia.