Wednesday, June 2, 2010

shukrani kwao pia

ni shukrani kwa kwenda mbele. baada ya lawama za muda mrefu kwao, leo nawashushia shukrani baada ya kufikiri positive.

napenda kumwaga shukrani zangu kwa walionilea. nililelewa na watu (wazazi) tofauti ambao kila mmoja anastahili shukrani kwani kila tendo nililotendewa linanipa fuzo kuubwa maishani.

wapo walionitukana matusi ya nguoni na kunitukania mama yangu mzazi nikiwa bado mtoto mdogo (hivi sasa nikikutana nao huwa najiuliza kama kweli wanayakumbuka matusi yale), lakini kuna jambo nililojifunza kuwa sio vyema kuwatukana wengine na hasa watoto wasiokuwa hatia eti kwa sababu una tofauti na mama zao. Ni somo hili, nawashukuru

wapo walionikwida na kunichapa viboko, makofi, mateke, ngumi na matusi juu, yaani kuna aliyejisikia kunitwanga tu bila sababu, nao nawashukuru kwani wamenifundisha jinsi mtu anavyojisikia akionewa au akipigwa, nawashukuru pia kwa somo hilo

wapo walionikacha walipoamini nahitaji msaada wao, nawashukurupia kwani wamenielimisha mengi juu ya kufanana na kufaana.

ninazidi kumwaga shukrani kwa yoote, kumbe tunajifuza mengi maishani kwa kutendewa lolote lile

hata katika siasa, negatives za watawali ni mtaji kwa wapinzani, NAWASHUKURUNI WOTE

5 comments:

Fadhy Mtanga said...

Posti ya leo imebeba ujumbe mzito sana. Ni kweli kabisa wale waliotu-treat visivyo mapenzi yetu ndiyo waliotushepu na kuwa hivi tulivyo leo.

Mija Shija Sayi said...

Yeeeeeees! Kakangu Kamala sasa umekomaa. Hiyo safi sana.

Ubarikiwe.

Yasinta Ngonyani said...

Kamala nakusifu kwa kufanya hili. Kwani ni muhimu sana kuwashukuru waliotulea hata kama walitulea visivyo usirudishie nawe pia . Upendo daiama!

Bwaya said...

Pamoja-:(

chib said...

Mh..... au ndio maana nawe unakuwa una-mtazamo wa hasi (negative) kwenye komenti, naona shukrani ni mambo yaliyokuwa kinyume na matarajio.
Kwa mtazamo wangu naona bado una hasira na matatizo yoooote yaliyopita. Wakati mwingine toa na shukrani nyingi kwa yale yaliyokuwa mazuri.