Friday, June 4, 2010

shurani kwa Munga, Mike, Andreas na Sant Baljit Singhkatika shukrani zangu za msimu huu nawakumbuka watu muhimu pia walionifanya nipege hatua, nibadilike na niwe mtu mpya. najivunia utu wao, najivunia huruma zao, upendo, mshikamano na kujitolea kwa ajili ya kupata mazuri mimi. hawa walinihangahikia na kunitesekea mpaka nikawa kiumbe mpya wa mafanikio


nikiwa kama kijana nilikuatana na changamoto za kifamilia, kimaisha na kidunia. nikawa mlevi na vurugu kibao. nilikuwa katika ugiligili nikijiuliza kama niuache mwli kwa hiari (nijiue) lakini hali ilibadika pale kijana Mc Donald aliponiunganisha na Hayati Munga Tehenan. nilikimbia ofisini kwa Munga na kununua vitabu vyake vyoote na akanikaribisha kwenye madarasa ya utambuzi


ni kwa kuhudhuria madarasa yale nikabadilika kabisaa mitizamo na kuanza kuwa positive na ndiyo maana ninatoa maarifa haya bure kwani yaliponitoa napafahamu mwenyewe. ajabu madarasa yale yalitolewa bure wakati katika mataifa makubwa kama Marekani hutolewa kwa gharama kuubwa sana na Munga mwenyewe aliyapata kwa gharamu kuubwa pia, ni utu ulioje huu kusahau gharama ili kunufaisha wengine?


ndipo akaja kijana Mike (michael) mahenge niliyesomanaye IFM na kunitambulisha katika meditation iitwayo santmat, nikakutana na sharti la kutokula nyama wakati maishani sikupenda kula hiyo nyama toka nikiwa mdogo. akashirikiana na Adam, Naju na mmarekani Vanessa kunielimisha na kunipatia vitabu na DVD, mwishowe mjerumani Andreas akanipatia 'initiation' bure kwaniaba ya master wa santmat yaani sant Baljit Singh.


ni kwa meditation hizo au sala za uzingativu nawezakuzishinda nguvu hasi, kuwa mtu mwema kadiri ya mtizamo na mafunzo ya santmat, naweza kuwa kijana mtanzania na ninaweza kuwashauri wenzangu. nazidi kukua kiroho na kuelekea kwa Mungu, ni furaha na ni fahari pia, najivunia kila aliyefanya juhudi hizi, nafaruhia maisha haya na kujiuliza kamasio wao nigekuwaje??


Ni shukrani kwao pia. NAWASHUKURU SANA

7 comments:

Mija Shija Sayi said...

Kamala Mungu ni nani?

Tukiachana na swali hilo, Ubarikiwe kwa yote mazuri uyatendayo. Maisha ndivyo yalivyo, katika uzoefu wangu wa maisha nimegundua kwamba hata ukiondokewa na wazazi wako mapema kiasi gani Mungu yuko nawe popote uendako, utaharibu, utaharibikiwa, utatibua watu, utatibuliwa na watu, utaanguka, utaangushwa, halafu mwisho kabisa utanyanyua mikono utasema bwana wee na liwalo naliwe. Hapo sasa ndipo utakaposhangaa Mungu anavyojitokeza. Si unaona hata wewe kina Munga, Mike, andreas na Sant Baljit Singh walivyotokea mwishoni kabisa. Achana na hao si unaona Mungu alivyokupa Mke Mwema? na bado mtoto anakuja, huyu ndo atakufuta machozi kabisa.

Ubarikiwe.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

duh!

yaaaa! ni wengi walofaidika!

Nuru Shabani said...

Elimu niliyoipata kwa Munga ilinifanya niwe mtu wa tofauti sana, sikufikia hatua ya kuwa mlevi kama rafiki yangu Kamala ila nilikuwa napenda sana kufikiri vibaya hadi ninayona maisha hayana maana tena. Namshukuru sana Munga popote alipo,aliweza kunionyesha upande mzuri wa maisha na kuyafurahia maisha katika hali yeyote ile.Shukrani kwake

Tandasi said...

kila la heri

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@damija, swali la Mungu ni nani nitalijibu, hiki ni kiporo cha pili kwako, uliwahi pia kutaka kujua sana juu ya meditation na kuna kiporo kingine. vyoote nitavijibu kila kimoja kwa wakati wake hata kama kwa kuchelewa. uliyoyasema yana ukweli mwingi sina cha kuongeza. kama ulivyosema wanakuja mwishoni na kamani nilivyowahi sema ni shule ambazo lazima tuzipitie zikiwa na koti la ugumu fulani kwani baada ya hapo tunaelemika

@chacha unaelewa kila kitu mkuu
@Nuru, yule jamaa alitutoa mbali

@Tandasi, karibu

katawa said...

Kama Munga na wqengineo wasingekuwapo nawe pengine usingekuwepo.Wale wapo na walikuwepo kwa sababu watu kama wewe mpo.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

katawa, ujumbe wako unafikirisha na ni changamoto pia kwamba kama sio watenda dhambi basi Kristo asingekuja