Monday, June 7, 2010

unaponyimwa kitu au kushindwa.

kuna kunyimwa, kuna kushindwa, wahaya wana msemo kwamba akunyimaye pombe amekuokoa na adha za ulevi.

hivi majuzi nilitaka kutume email kwa mtu, ikakataa ku-attach, kesho yake nikagundua kuwa ile doc.niliyotaka kuattach ilikuwa siyo kamili na ingeniharibia kazi zote, shukrani kwa mtandao kugoma.

hii yanikumbusha mbali pia, kuna muuzaji alikataa kuniuzia maji bila sababu, nikaenda kuomba kwa mdada nisiyemjua, akageuka kuwa mke wangu.

kuna vitu vingi vinaonekana kukataa kushindwa, nasi tunapaswa kuangalia upande mwingine badala ya manun'unikoz mengi u siyo wakuu????

ni ujumbe wa leo

4 comments:

Candy1 said...

Ndio hawa watu wanasema "things happen for a reason". Mimi sana huwa namiss basi kwenda sehemu halafu nakutana na mtu niliyepoteana naye kwa muda mrefu, so yh...ujumbe mzuri na kweli kabisa

Munale said...

Sana tu,Kamala jumbe zako huwa
nazikubali sana.Big up

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

munale, shwari?? nilikuwa
Musoma hivi karibuni lakini sikukutafuta, mwmishoni mwa juni tutaonana

Anonymous said...

du bro mi ndo leo naona blog yako na honest nimejifunza kitu, kuna kitu nataka kukifanya lakini out of no where nahisi sitaki tena kufanya kitu hiko haka ka ujumbe kamenitia moyo pengine kuna kitu kizuri zaidi ya hiko ambacho mungu atanipitisha kwacho
thanx.