Thursday, July 8, 2010

amri hii, waheshimu baba yako na mama.........

"Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako"

hili ni andiko katika biblia kuwa usipo waheshimu bila shaka siku zitakuwa kidogo sana au??

ila najiuliza itakuwaje na au inakuwaje kwa wale waiopenda kuishi siku nyingi. andiko hili linadhbitisha ya kuwa biblia iliandikwa na wazee walioogopa hatima yao lakini pia iliandikwa enzi zile watu wanapenda kusihi sana

sasa amri kama hii unamwambia kijana ambaye kachoshwa na maisha na anatamani kufa, si atawadharau ili siku zipungue fasta. lakini je ni kweli kwamba wanaoheshimu wazazi wao huishi siku nyingi? na je kuishi siku nyingi kuna faida gani kwa aishiye?

2 comments:

Bwaya said...

Naam. Umenifikirisha zaidi.

Yasinta Ngonyani said...

Kamala ni iimani yako. ukiamini basi itakuwa hivyo.