Wednesday, July 14, 2010

jibu kwa Damija; Mungu na upendo ni kupendana

katika kuangalia tena juu ya upendo. najikuta nikiwa sina definition ya kutosha ya kiswahili juu ya upendo ninini.

laikini kumpenda mtu ni kumkubali na kumpokea kama alivyo. ili tumjue Mungu, tunalazimika kuwa na upendo. sio upendo kwa Mungu pekee bali kwa kazi zake zote. "upendo na heshima kwa kila kiumbe cha Mungu" ndiyo njia kuu ya kupenda. nilazima nijipende, nikupende naunipende ili kukamilisha amri hii ya maumbile.

ukinipenda basi hutayajali sana mapungufu yoyote ntakayokuwa nayo kwani unanipenda. ukinipenda, utanithamini utaniheshimu na utaniamini na upendo yatupasa kumkubali kila mtu na kila kitu kama kilivyo.

penye upendo kuna kuamniniana na penye kuaminiana kuna amani na penye amani kuna urafiki, umoja na maelewano.

sio kupendana sisi tu bali na vitu vyote vilivyokaribu yetu. hatupaswi kuwa watu wa kulalamika. kwa mfano mvua ikinyesha, unalalamikia matope, kulowa nk. na jua likiwaka, unalalamikia kuungua, kuumia macho nk. na yatandapo mawingu, basi wewe unalalamika kwamba siku haieleweki, sio mvua sio jua yaani unaboreka. huu sio upendo na sio heshima kwa Maumbile na pia twazijaza fikra zetu mambo mabaya na sisi twawa wabaya pia.

ndio maana ukikuta wanampiga mwizi nawe unajiunga kumpiga bila kujiuliza maswali na hivyo tayari unahasira zako za kumallizia kwa mwizi badala ya kuwa na upendo wa kujua kwamba naye ni binadamu kama wewe, labda kasingiziwa na labda ........

Maumbile au Mungu ndiye mfano mkuu wa upendo. angalia jua liwakavyo kwa watu wote, mvua inyeshavyo, maji yatirirkavyo na kadhalika.

tukipenda tutazaa matunda mema na tusipopenda basi sisi tutakuwa wasio na maana.

hebu jaribu kupenda harafu uone furaha utakayokuwa nayo. chukulia kiurahisi kila kitu. umekosa chakula, wewe jiambie kwamba labda ilibidi leo nifunge. umekosa usafiri jiambie kwamba labda ilibidi leo nifanye zoezi kidogo la kuutembea, utaona amani itakayokujia.

duniani tumekuja kutoa upendo kuliko kupokea. ni lazima tutoe upendo bila malipo wala kudai malipo kwani tupo ili kutoa upendo huo. angalia miti itoavyo matunda bila kujali inamtolea nani, yenyewe ni kutoa tu. ardhi itoavya mimiea lukuki, miti inatoa kivuli, hewa safi upepo nakadhalika bila kujali inamtolea nani. yenyewe imekuja kuotoa.

tusipopenda nakutoa upendo au tukipenda kwa masharti, basi tutakuwa kama mti usio zaa matunda wakati wa njaa na wala usiotoa kivuli. tutakuwa kama mto utaoya maji machungu yasiyofaa kunywewa na hivyo yatupidi kulaaniwa. upendo ni muhimu sana kwetu kuutuo na kumuka hatuwezi kupendwa kama hatupendi

mwenzako akikukanynaga kwenye gari, basi jiambie kwamba ni bahati mbaya badala ya kumrukia. nakumbuka siku moja nilijikwaa na kudondoka, nilicheka na kushangaa kwa kujiuliza mara ya mwisho nilidondoka lini, sikuweza kukumbuka na hivyo nikasema 'siku nyingi sijaanguka ehe' nikainuka kwa amani na kwenda kuwasimulia wenge kwamba leo nimejikwaa na kuanguka tena.

sijui niseme nini lakini huu ndio mtizamo wangu juu ya kitu kinachoitwa upendo. jipenda, jikubali na jipokee kama ulivyo kwani ni wewe na ulivyo umekamilika!

kama dini zetu au angalau moja ingeweza kuapenda waumini wake bila kuwatenga, basi tusingekuwa na dini kibao kwani upendo ungetuvutia kwani upendo kawaida yake ni kuvutia vinavyo/wanaotafuta kupendwa.
MIMI NAKUPENDA. UNIPENDE USINIPENDE HAINIHUSU, KAZI YANGU NI KUKUPENDA TU. i LoVE u

No comments: