Friday, July 16, 2010

kuhusu salamu, kuna maoni haya, tuyajadili

Yesu alitumia salamu kama 'amani iwe kwenu' 'amani iwe nanyi' nk. Ni kweli waumini wa leo tumekuwa na salamu za aina nyingi, pamoja na hayo bado salamu hizi zinalengo moja la kumwinua YESU kama Bwana wa mabwana. Ikumbukwe kuwa Yesu asingesema " BWANA YESU ASIFIWE" au "BWANA ASIFIWE" au " TUMSIFU YESU KRISTO" kwa sababu yeye akikuwa MUNGU kamili na asingeuza wazifa wake kwa kumsifu ama kumwinua malaika au kiumbe mwingine. Yeye ni ALFA NA OMEGA, hakuna aliye juu yake.

Kuhusu shikamoo, ikumbukwe kuwa tunawaenzi wakoloni. Ukisoma historia ya biashara ya watumwa, utaona jinsi shikamoo ilivyotumiwa na watu wa jamii ya ASIA, na kwa kiarabu shikamoo ina maana ya "NIKO CHINI YA MIGUU YAKO". Hii ilitambulisha ukuu na mamlaka ya Sultani kuwa siku zote yuko juu. Salamu hii hata mimi hainipi amani kabisa, mara nyingi imetumiwa vibaya na baadhi ya watu ambao kisaikologia hupenda kuwa juu ya wengine na kuilazimisha shikamoo hata kama kiumri ni wadogo kuliko mtoa shikamoo.

Mfano utasikia mtu anaitikia 'marahaba' kutokana na mazoea wakati kasalimiwa....habari yako,....za sahizi...!.

Mtazamo wangu ungependelea salamu zisizo ambatana na shikamoo. Turudi kwenye dhima au maana ya salamu kuliko kuangalia utambuzi wa umri ili upewe shikamoo.

Pia ikumbukwe kuwa sio rahisi kwa kila mtu kumtambua umri wake kila unapokutana nao ili uamue kutoa shikamoo ama la!

"BWANA YESU ASIFIWE"

1 comment:

chib said...

Pamoja na kuwa mada ni nyingine, lakini Mkuu nakupa hongera kwa kumuongeza Kamala mwingine!