Thursday, July 29, 2010

mapenzi, mapenzi ni matamu na machungu labda ehe?

jamani ukikumbukia labda enzi zako zilizopita kwenye mapenzi unakutana na visa na mikasa kibao. simu hupigwa na wengine hubusu kwenye simu, kila mtu huelezea hisia zake kwenye simu kwa waliokaribu na waliombali. humlazimisha mtu kusogea mbali na kadamnasi ili siri zake kwa mpenziwe zisisikike, kumbe siri zenyewe kwa asiyehusika ni ujinga mtupu

nimekumiss nk nk

hufika hatua mapenzi yakawa sio mapenzi. wengine hulia jinsi walivyohumizwa, kumbe kuondoka kwa mpezi wako ni hatua nzuri ya kuanza kuishi maisha yako na atakuja mwingine, utakayempenda zaidi naye akakupenda zaidi ya yule aliyetangulia, ukishikilia zile za niliumizwa unajiumiza mwenyewe, kumbuka kuna anayekupenda zaidi na mabadiliko ni muhimu ili tujifuze

vinnginevyo mapenzi na mpenzi ni muhimu kuliko hata wazazi au ndugu. eti kama mpenzio kalazwa, na wazazi wako au nduguzo wamelazwa, unapaswa kuwajulia khali, utaenda wapi?? kwa mpenzio bila shaka hata kama labda mpenzio yuko hospitali ya mbali na wazazi au ndugu wako karibu, ni mapenzi jamani, ndio chanzo cha ongezeko la watu!!!!

2 comments:

nyahbingi worrior. said...

......hufika hatua mapenzi yakawa sio mapenzi. wengine hulia jinsi walivyohumizwa, kumbe kuondoka kwa mpezi wako ni hatua nzuri ya kuanza kuishi maisha yako na atakuja mwingine, utakayempenda zaidi naye akakupenda zaidi ya yule aliyetangulia, ukishikilia zile za niliumizwa unajiumiza mwenyewe, kumbuka kuna anayekupenda zaidi na mabadiliko ni muhimu ili tujifuze......

Ujumbe tosha kaka.Ahsante.

Tandasi said...

naam baada ya shule nimerudi kwa upya habari kamala MUNGU AKUBARIKI asante kwa kaujumbe kazuri UDUMU UMOJA