Saturday, July 3, 2010

matangazo ya vilevi na kisicho sahihi


bila shska unaangalia na kuona baadhi ya vitu vinavyoendelea kwenye vyombo vyetu vya habari katika matangazo mbali mbali. tunaishi katika jamii ambayo imegeuka ya kudanganywa na kupotezwa.

naagalia vyombo vya habari katika matangazo mbali mbali na hasa haya ya kombe la dunia lakini hata yale ya kila siku
unaona jamaa wanapumbaza (brainwash) watu kwa matangazo ya kuuza vitu 'haramu' kuwa sio haramu na ni maisha bora.

ukiangalia jamaa anakwambia kuwa ukinywa kilevi fulani utafnikiwa au uvutaji sigara ndio maisha.
au burudika. nafikiri hata kama bangi na madawa ya kulevya vingelipiwa kodi basi vingeruhusiwa.

mimi sichukii vilevi kwani kuna wanaovipenda, lakini matangazo ya vilevi hivi yawe ya kusema ukweli na sio ya kuwaambia watu kisicho kwani huwapoteza vijana kwa njia hii.

1 comment:

chib said...

Sasa huyo mtoto anakunywa mlamba uliowekwa kwenye chupa ya safari au ndio kilevi chenyewe??!!
Matangazo ya sigara humalizia kwa kutoa onyo kuwa uvutaji wa sigara unaweza kukuletea madhara, lakini watengenezaji hawaachi kutengeneza, na wavutaji wanaongezeka tu. Kama ulivyosema... chochote kinacholipiwa kodi basi si haramu, nina hakika madawa ya kulevya yakianza kutozwa kodi, basi hakuna tena kuharamisha.