Tuesday, July 20, 2010

mtoto kazaliwa, tarehe ile ile ya kuzaliwa kwa baba

ilikuwa ni usiku wa kuamkia Jumamosi, mke wangu analalamika tumbo, namuuliza vp, anasema hajui, tunavumilia kuwa labda asubuhi tutampeleka kwa wataalamu. halali, anahangahika, hata mimi silali, ni mishale ya saa nane usiku.

naamua kwenda kwa bibi mmoja jirani amabaye kafika kumwona kijana wake, ni mkunga wa jadi, lakini kuna shemeji yangu pia hapa nyumbani. wakimuona mke wangu, wakabwatuka "ndo uchungu wenyewe, ondokeni haraka" ni saa kumi hivi, giza nene, nahaha kutafuta usafiri, nimeshauriwa kwenda Mugana hospital, iliyoko umbali kadhaa kutoka Bukoba mjini ninakokaa kwani hosp ya mkoa sio nzuri kwa wazazi na uzazi.
tafuta gari, jirani zangu wana vigari vidogo, bara bara yenye mashimo ni nongwa kwavyo. natafuta gari la ofisi randcruiser ili kuwahi, mkuu haamki, naenda kwa msaidizi wake, cruiser inakuja, haoo hospitalini, twafika alfijiri kama saa kumi namoja.


walinzi wametupokea vizuri, wanatwambia atajifugua mchana au jioni, mpaka jioni, basi watwambia usiku, haikuwa.
ninashuhudia live uchungu na sasa naelewa nini maana ya uchungu wa mwana kuujua mzazi. mama anahangaika, manesi wakiingia wodini, natoa taarifa kwa kiherehere kuwa uchungu ushaongezeka, wananicheka na kuniambia kuwa mtu akiwa na uchungu, hawezi kulala kitandani, nawauliza atalala wapi? wananijibu utaona tu.


saa sita usiku, wanampeleka labour, nikishuhudia, labour yenyewe haiko mbali na wodi yetu, nasikia kila kitu. navumilia na kudhibiti hisia zangu kiutambuzi. nawauliza manesi wanadai bado tu. wananiambia mwanamke ni jasiri, anaenda labour kwa miguu na sio kwa kubebwa wala nini.

duh kidume nashuhudia. mida ya saa kumi na mbili asubuhi nasikia sauti zinazoashiria mtoto kuzaliwa. anaitwa shemeji yangu apeleka khanga / vitenge, anarudi na kuniambia mambo tayari, amekaona katoto!! ni saa kumi na mbili na dakika nne, ila simwamini, namwona chizi.

ghafra atoka nesi akiwa na gloves, ananpongeza, ni mtoto wa kiume, ana sura / uso mrefu, kwa kifupi sura yake na yangu havina tofauti, ni mimi mtupu. ni furaha isiyonakifani, naingiza mkono mfukoni na kutoa pesa zilizomo, ni Tsh 10,000 na kuwapa manesi kama takrima, walimsaidia mke wangu, natamani kuwapa zaidi hata kama wako kazini na wanalipwa kwa kazi hiyo

ghafra mke wangu aja wodini, namkumbatia kwa furaha isiyona na kifani, natokwa na machozi nalia kwa dakika kadhaa, nampongeza, nafurahia, mwenyewe kachoka anastahili kupumzika. katoto kanaletwa kalale na mamaye kapate kula chakula kitokacho mwilini mwa mama,nifuraha isiyo nakifani

pamoja na usingizi na uchovu, nahudhulia ibada kwenye kanisa la KKKT. wodini napongezwa na kila mmoja
ni mtoto wa kiume aliyezaliwa tarehe kumi na nane mwezi wa saba (18/7/2010), ni tarehe iyo hiyo aliyozaliwa marehem baba yangu, nakumbe ni yamandela. jina la mtoto bado. nilianza kumheshimu mwanamke toka zamani ila hii inaongezea heshima kwa mwanamke

10 comments:

Munale said...

Hongera Kamala kwa kupata mtoto wa kiume mnayefanana,kwa hiyo utamuita
jina gani?

Yasinta Ngonyani said...

Nimefurahi sana kusoma habari hii nimetoa hadi mchozi wa furaha kimawazo nimewaona jinsi mlivyo na furaha. Hongereni sana na nawatakieni kila la kheri kwa malezi mema kwa mtoto wetu. Msalie salamu kutoka kwa shangazi Yasinta:-)

Mija Shija Sayi said...

Na mimi nilipoanza kusoma sentensi ya kwa tu, machozi yakaanza, maana ile shughuli Muumba ndiye anayejua.

Hongereni sana, naomba umuulize wifi ataongeza lini wa pili uone jibu lake...

Kila laheri jamani.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Munale: atamuita Joti!!!!!

Da Mija: Of course akimuuliza anaweza hata kumchoma kisu hivo namshauri asubirie baada ya majuma 10 or so halafu atajua lini wa pili anaingia.

Niliwahi kushuhudia mdada akiapa kuwa hatazaa tena wakati akiwa ktk uchungu na akawa anamtukana alosababisha hiyo hali na kusema hataki kumuona tena!!!!

Cha ajabu baada ya kujifungua akawa wa kwanza kumuulizia 'fulani yuko wapi?' na alipofika hakukuwa na tusi wala nini!!

Sitaki nataka eti, eh!!!!!!

Da yasinta na Mija, nanyi huwa mnalaani ama?

lol!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Hongera Mulangira na ninawatakieni kila la heri...

Nakumbuka binti yangu wa kwanza alipozaliwa manesi na madaktari "waliniingiza mjini" walipofanikiwa kunifanya niende kushuhudia shughuli hii ya uzazi. Na kweli sitasahau na kutoka siku ile heshima na upendo wangu kwa wanawake - na hasa mamangu vilibadilika. Kwa mtoto wa pili na wa tatu, nilikataa kabisa kuingia katika chumba cha uzazi - kitendo ambacho manesi na madaktari walikishangaa.

Hongereni tena na tena. Mungu Akabariki kamalaila kake kakue salama na kuwa kanautambuzi maarufu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@munale, bado sijapata jina!!!
@damija, duh!!!
@chacha, huyo jamaa namfa...
@matondo, ni kweli ila mimi ujasiri wa kuingia tena leba bado upo tu. kuwa kanautambuzi!?? nitaliombea na kujaribu kulifanikisha hilo, japo kana karma zake, mapenzi yake na malengo yaliyokaleta duniani

Blackmannen said...

Hongera sana Kamala na Mama Kamala kwa kupata mtoto. Siku zote ni furaha kubwa sana watu wa ndoa wanapopata mtoto.

Mapenzi huongezeka kuliko hata siku ile mlipoonana kwa mara ya kwanza. Neno la kuwa "Nafsi Moja", siku kama hiyo hutimia.

Kamala msipate taabu ya kutafuta jina la mtoto, ni "BlackMadiba Kamala".

Hiyo ni kwa sababu kazaliwa tarehe ya watu Mashuhuri duniani "Nelson Mandela" - Madiba na Black=Blackmannen, na kwa kuongezea Marehemu Babu yake naye pia alizaliwa tarehe kama hiyo.

Kwa maana hiyo, ameongezeka mtu Mashuhuri mwingine wa tatu duniani katika kuzaliwa tarehe hiyo, na tutajiita "Three The Hard Way". Duniani hapatatosha!

It's Great To Be Black=Blackmannen

Anonymous said...

MTOTO MWITE MUSHOBOROZI KAMA WEWE UNAVYO SHOBOROLA WATU AU SIO BATAMWA DSM 0769 505216

SN said...

Kamala, ingawa hatufahamiani (ukiacha kukutana kwenye blogs), napenda kukupa HONGERA!!!

Hajapewa jina tu??

Tandasi said...

mtoto aitwe LUTAKAMALA